Na Stahmil Mohamed
Kutokana na uchache wa watalii kutoka China kuja Tanzania,
sasa Tanzania imeamua kushirikiana na China kwa lengo la kuboresha soko
China sambamba na kuangalia ni maeneo gani wanaweza kushirikiana ili
kuweza kukuza na kutangaza soko la Utalii Tanzania.
Akiongea na vyombo vya habari Leo katika mkutano
ulioandaliwa na ubalozi wa China kwa kushirikiana na TTB uliofanyika
katika ukumbi wa Julias Nyerere jijini Dar es salaam, mwenyekiti wa bodi
ya Utalii Tanzania amesema kuwa uhusiano wa China na Tanzania ni wa
muhimu sana na wanampango wa kubadilisha mfumo ili wachina waingie kwa
wingi nchini sambamba na kuboresha soko la Utalii nchini China.
Pia amesisitiza kuwa fursa hii ni nzuri sana ikitumika
ipasavyo kwani wamepata nafasi ya kuwatumia watu maarufu kutoka nchini
China ili kusaidia kutangaza Utalii wa Tanzania na kusema kuwa moja ya
watu maarufu watakaotumika kama mabalozi wa kutangaza Utalii ni
muigizaji maarufu kutoka China anayejulikana kwa jina maarufu la
'Maudodo' pamoja na Dkt anayetunza sokwe mkoa wa kigoma na kusema kuwa
wameamua kutumia wazo hilo kwa sababu wana mvuto kwenye jamii.
Pia ameongeza kuwa bodi ya Utalii nchini iko tayari
kushirikiana bega kwa bega na China ili kwa pamoja waweze kufikisha soko
la Utalii mbali na kuwa la kimataifa kwani Tanzania ina kila aina ya
vivutio vya kipekee ilivyojaliwa na ni vya asili kabisa.
Aidha kwa upande wake katibu wa Maliasili na Utalii
Gaudence milanzi amesema kuwa wameamua kushirikiana na China kwa sababu
China ni watu wanaosafiri sana duniani kote hivyo itasaidia kwa kiasi
kikubwa kuutangaza na kutengeneza soko la Utalii nchini.
Pia Milanzi ameipongeza China kwa kupiga marufuku bidhaa
zinazotengenezwa kwa kutumia malighafi ya meno ya tembo na faru na
kusema kuwa ni jambo jema kwani itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza
ujangili na kuzihasa nchi nyingine kufuata uamuzi kama ilioufanya China.
No comments:
Post a Comment