• Breaking News

    ..

    ..

    Monday 26 March 2018

    BAKWATA WAZINDUA KAMPENI YA HIIJA

    Baraza la waislamu nchini, BAKWATA leo limezindua rasmi kampeni ya maandalizi ya safari ya hijja kwa mwaka 1439 ambapo ni sawa na mwaka 2018.


    Akizundua kampeni hiyo Mufti Mkuu wa Tanzania Shekh Abubakari Zuberi amewashukuru watu wote ambao wanaofanikisha maandalizi ya safari ya kwenda kwenye ibada hiyo maalum ingawa kuna changamoto mbalimbali ambazo zinajitokeza.


    Pia amesihi taasisi na vyombo vyote  ambavyo vinasimamia kushikamana ili kuboresha mahitaji yote ya Mahujaji ambao wataenda kutekeleza ibada hiyo.


    "Kazi hii haitakiwi kulala, inahitaji ukweli, kuwafundishwa, kuwaelimisha Mahujaji pia kufanya kwa ajili ya radhi za mwenyezimungu ili mambo yote yaende sawa" amesema Shekh Zuberi.


    Aidha ametoa rai kwa wale wote ambao wataenda kuhijji kuwa wapole, wenyenyekevu, wasikivu na kufuata taratibu zote kutoka kwa wasimamizi pindi wanapoenda kuhijji ili  kuepuka usumbufu unaojitokeza mara kwa mara.

    Kwa upande wake kamishina wa uraia na pasipoti Gerad Kihinga amesema kama serikali watahakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha safari hiyo.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI