• Breaking News

    ..

    ..

    Monday 26 March 2018

    DC Mjema awndesha Zoezi LA upandaji Mti Katika Hospital Ya Mama na Mtoto

    Mkuu Wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema Amefanya Zoezi LA kupnada mti katika Hospital ya Mama na Mtoto Iliopo Chanika

    Aprili 01 ya kila Mwaka ni Siku ya upandaji Miti, leo hii Tarehe 26 Machi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema amefanya uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti kwa kupanda mti katika Hospitali ya Mama na Mtoto iliyopo Chanika ikiwa ni njia moja wapo ya kuhamasisha upandaji wa miti kwa Wananchi na Viongozi wa Manispaa ya Ilala.

    "Natoa wito kwa kila mmoja wetu kupanda miti katika maeneo yanayomzunguka. Vilevile napenda kutoa wito kwa Viongozi wa Halmashauri kuhakikisha kwamba miti inayopandwa mwaka huu inatunzwa na kukua ili zoezi zima la upandaji miti liwe na tija" alisema Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema wakati wa zoezi la kupanda mti.

    Ikumbukwe, kwa mwaka huu wa 2018 siku ya upandaji miti imebeba kauli mbiu isemayo "Tanzania ya kijani inawezekana, panda miti kwa maendeleo ya Viwanda" maudhui ya ujumbe huu ni yanalenga kusisitiza Waananchi katika Miji na Vijiji, kudumisha matumizi endelevu ya Misitu kwa kizazi kilichopo na kijacho

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI