• Breaking News

    ..

    ..

    Monday 26 March 2018

    Kongamano la katibu mkuu CUF halikuwa la chama

    Katibu wa wilaya ya kinondoni wa chama cha CUF Mohamed S.Mkandu ametoa taarifa sahihi juu ya kongamano lililofanyika katika kata ya Tandale lililohudhuriwa na katibu mkuu wa chama hiko Maalim Seif Sharifu Hamad halikuwa kongamano la chama ila walitumia neno chama ili kutimiza malengo yao binafsi.

    Akizungumza na waandishi wa habari bw.Mkindu amesema kongamano hilo halikufuata taratibu za chama na hasa ujio wake katibu mkuu upo nje kisheria kwa mujibu wa katiba ya chama hiko.

    "Jambo lolote kiongozi wa juu atakalolifanya katika ngazi zake za chini ni lazima awasiliane na katibu mkuu wa wilaya husika ili maandalizi muhimu yaweze kufanyika pamoja na kuhakikisha usalama wa kiongozi huyo" amesema Mkindu.

    Aidha amesema katibu wa wilaya ndiye anayetoa taarifa kwa vyombo vya usalama vya nchi kwa ajili ya kuimarisha usalama.

    "Lakini kinyume chake siku hiyo mawasiliano hayakufanyika mimi katibu mkuu wa wilaya kinondoni sikuwa na taarifa yoyote ile ya kongamano na pia ujio wa katibu mkuu Maalim Seif Sharif Hamad"amesema Mkindu.

    Sambamba na hayo Mkindu amesema katika uchaguzi uliopita kuna baadhi ya wanachama na viongozi wa matawi,kata na wilaya wamekisariti chama kwa kumuunga mkono na kumfanyia kampeni mgombea wa Chadema Salim Mwalim na tayari wameshaanza kuchukua hatua za kinidhamu .

    Pia amesema baadhi ya viongozi wa chama hiko wamefukuzwa na kuvuliwa uongozi wao ambao katika Kata ya Tandale mwenyekiti Blandina mwasabwite,katibu wa Tandale Ally Mtumweni,Kata ya makumbusho Mwenyekiti Pamela Farahani,mwenyekiti wa tawi Mwananyamala Mashaka Adamu,Mwekahazina Halid Magwai,m wekahazina Tawi la mchangani,kata ya kigogo-Katibu Halidi Sungura,kata ya ndugumbi katibu Seif,kata ya magomeni mwenyekiti na katibu pia bado wanaendelea kuwachukulia hatua za kinidhamu wengine watakaobainika wakisaliti chama.

    Kwa upande wa mwenyekiti wa tawi la alfonso drakama Tandale CUF bwn.Said M.Makame ambapo Maalim Seif Sharif Hamad alitembelea amesema yeye kama mwenyekiti hakuwa na taarifa hiyo ya ujio huo wa katibu mkuu wa chama hiko.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI