• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday 27 March 2018

    Walimu na wanafunzi kupata mafunzo ya kisayansi na teknolojia

    Katika kuhakikisha nchi inakuwa na wanasayansi mahili Taasisi ya Youth Scientists Tanzania imeandaa onesho maalum Kwa ajili ya wanafunzi wa sekondari ili kuweza kuonesha umahili walionao katika ugunduzi wa kisayansi na kiteknolojia.


    Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Mwanzilishi mwenza wa Taasisi hiyo Dr Gosbert Kamugisha amesema kuwa onesho hilo litakuwa na wanafunzi 200 na walimu 100 ambao watapewa mafunzo kuhusu namna ya kutengeneza kazi zao za kisayansi.


    Ameongeza kuwa onesho hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 1 hadi 2 mwezi agosti mwaka huu,huku wanafunzi watakaofanya ugunduzi mzuri watapewa pesa taslimu,medali ,vikombe na uimarishaji wa maktaba ya shule yao.


    "Kama tulivyofanya kwa miaka sita iliyopita karimjee jivanjee foundation watawazawadia wanafunzi zawadi ya udhamini wa masomo ya chuo kikuu ili kuwawezesha kusoma masomo ya sayansi na teknolojia katika ngazi ya chuo kikuu",alisema.


    Aidha amewataka wanafunzi ambao watakaoshiriki katika onesho la mwaka huu kutuma kazi miradi yao kabla ya Aprili 21

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI