Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala
imepitisha bajeti ya sh.bilioni 287 katika mwaka fedha wa 2018/2019 ikilinganishwa bajeti iliyopita ya 2017,2018
ya sh.bilioni 124.
Akizungumza na waandishi habari
jijini Dar es Salaam, Mchumi wa Manispaa hiyo, Ando Mwanduga amesema kuwa
bajeti hiyo katika sehemu kubwa ni kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Mwanduga amesema kuwa fedha hizo zitapatikana katika makundi mawili
ya ruzuku pamoja na vyanzo vya ndani ambapo hakuna mwananchi atakayeonewa
katika bajeti hiyo.
Amesema kuwa chanzo cha mapato ya
ndani ni wanatarajia kukusanya sh.bilioni 56.8 ambapo na fedha nyingine zitakuwa ni za ruzuku.
Mwanduga amesema kuwa kila diwani
anataka kuwa na mradi katika kata yake lakini haiwezikani kutokana na uwezo wa
manispaa.
Amesema kuwa bajeti hiyo
itatekelezeka ni pamoja na kuwa na vyanzo hivyo viwili vya ruzuku na mapato ya
ndani na asilimia 60 ni kwa ajili ya maendeleo ya wananchi katika kutekeleza
miradi.
No comments:
Post a Comment