Na Stahmil Mohamed
Wanawake sita wenye ualbino kutoka Afrika wamejipanga kukwea mlima Kilimanjaro wakiwa na lengo la kubadilisha mitizamo kwa jamii kuwa kutoka hali ya kuwa muathirika hadi kujengewa uwezo na kuifanya jamii kuongeza uelewa kuhusu waathirika wa mashambulizi ya ukatili dhidi ya albino.
Wanawake sita wenye ualbino kutoka Afrika wamejipanga kukwea mlima Kilimanjaro wakiwa na lengo la kubadilisha mitizamo kwa jamii kuwa kutoka hali ya kuwa muathirika hadi kujengewa uwezo na kuifanya jamii kuongeza uelewa kuhusu waathirika wa mashambulizi ya ukatili dhidi ya albino.
Hayo yamesemwa na kiongozi wa kikundi cha Climb of Albinism Jane Waitera alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na safari hiyo ya kupanda mlima Kilimanjaro ambapo amesema safari hiyo itakuwa mwezi wa tisa ya mwaka huu2018 nakuamini kuwa kwakisimama kwenye kilele cha mlima watakuwa wanatuma ujumbe madhubuti utakaosaidia kuelimisha jamii na kuondoa mitizamo hasi inayoeneza fikra mbaya kuhusu watu wenye ualbino kwakufanya hivo dunia itaona na kujifunza.
Aidha Shirika la Under The Same Sun linalotetea haki na ustawi wa watu wenye ualbino kwa kuelimisha jamii kuhusu ualbino linaunga mkono shughuli hizo za kupanda mlima na kuamini kuwa ipo siku moja watu wenye ualbino watachukua nafasi yao inayostahili katika Ngazi zote za jamii na kwamba siku za ubaguzi dhidi ya watu wenye ualbino zitakuwa kumbukumbu zilizofifia hivyo anaamini kuwa upandaji wa mlima huu itaionesha dunia kuwa albino ni watu madhubuti.
Naye mtengenezaji wa filamu na kiongozi wa msafara Bw Elia Saikaly amesema mara nyingi watu wenye ualbino wanaoneshwa kama waathirika hivyo wanampango wa kuvunja dhana hiyo kwa kufanya vitu ambavyo havijawahi kufanyika licha ya changamoto nyingi zinazowakabili na watawahakikishia jamii jinsi wanawake hao walivyo na nguvu, uwezo, na wawe mfano wa kuigwa kwa dunia .
Hata hivyo katika hatua hizo Zakupanda mlima ambazo zitakamilika kwa siku nane hadi kufika kwenye kilele wanatarajia kutoa simulizi mbalimbali kuhusiana na mapito mbali mbali ya maisha yao waliyopitia hadi sasa
No comments:
Post a Comment