• Breaking News

    ..

    ..

    Monday 26 March 2018

    CUF yajipanga kufatilia na kuwafichua wenye nia ya kukihujumu chama

    Chama cha wananchi CUF leo kimetoa maazimio ya kikao cha kamati tendaji ya taifa iliyokutana machi 25 mwaka huu katika ukumbi wa ofisi ya wabunge wa CUF uliopo magomeni, Dar es salaam chini ya uenyekiti wa katibu mkuu.


    Akiongea na vyombo vya habari katibu wa chama hicho Seif Shairf Hamad amesema kuwa,katika kikao hicho yalitolewa maamuzi mbalimbali kutokana na ajenda zilizokuwepo mezani ambapo kuhusu ajenda ya uhujumu wa chama cha CUF kamati iliamua chama kiendelee kufuatilia hujuma hizo kwa lengo la kudhibiti pia iliagiza viongozi wa ngazi zote kuwa makini na kufuatilia hila zote za kukihujumu chama na kuwafichua wale wote wanaopanga njama hizo.


    Aidha ameongeza kuwa katika ajenda hiyohiyo waliamua kuwahimiza wanachama kuimarisha umoja, ushirikiano na mshikamano  huku wakitambua kuwa umoja ni silaha mujarabu ya kuwashinda maadui wa chama.


    Pia amesema  katika ajenda ya taarifa kuhusu maendeleo ya kesi za  chama, kamati inawapongeza mawakili wanaokiwakilisha chama katika kesi hizo kwa kusimamia kwa dhati na kwa weledi wa hali ya juu na kuongeza kuwa kamati inawaomba wanachama hasa wanaoishi jiji la Dar es salaam na viunga vyake waendelee kujitokeza kwa wingi mahakamani kila siku ambayo kesi inasikilizwa.


    Kuhusu hali ya usalama nchini Seif amesema kuwa kamati iliamua kuendelea kufuatilia kwa makini malalamiko ya wananchi yanayotolewa kuhusu ukiukwaji wa haki zao kisha kushauriana na wadau wote ikiwemo serikali  ili kubaini ukweli wa malalamiko hayo na kubaini chanzo chake ili kutokomeza kabisa hali hiyo, kuikumbusha serikali kuwa jukumu lake la msingi ni kulinda usalama wa raia na mali zao ili jeshi la polisi na vyombo vingine vya ulinzi vijiimarishe kutimiza wajibu huo kwa weledi.


    Pia ameongeza na kusema kuhusu hali ya usalama nchini kamati iliamua kuwakumbusha wananchi watimize wajibu wao na kutetea hali na kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuwa na amani kwa kutofumbia macho vitendo vyote viovu vinavyoweza kuitikisa misingi madhubuti ya taifa letu, ikiwemo umoja na mshikamano.


    Sambamba na hayo amesema kamati ya utendaji wa Taifa ilitoa wito kwa watanzania wote kuwa kitu kimoja katika kutetea maslahi mapana ya nchi yetu na watu wake na kuendelea na utamaduni wetu wa kuhurumiana na kushirikiana katika wakati wa majaribu na wakati wa furaha.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI