• Breaking News

    ..

    ..

    Monday 26 March 2018

    Rais Magufuli Awafananishia viongozi hawa na vilaza

    Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kuwaambia viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuwa vilaza baada ya kugundua Mamlaka ya Chakula na Dawa, TFDA imekuwa kikwazo kwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD).

    Rais Magufuli amesema hayo leo Machi 26, 2018 wakati akizundua magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ambayo yanategemewa kuanza kusafirisha dawa mijini na vijinini, akiwa kwenye uzinduzi huo Rais Magufuli alipokea malalamiko kuwa zipo baadhi ya taasisi za serikali zimekuwa zikichangia kukwamisha ucheleweshwaji wa dawa ambazo zinaletwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD). 
    "Nimesikia saa zingine kunakuwa na ucheleweshwaji kati ya taasisi fulani fulani ndani ya serikali taasisi ya vyakula TFDA, mnaleta madawa halafu mnashindwa kupata kibali bandarini, madawa yanacheleweshwa inawezekana 'expire date' yake inafika madawa bado yamezuiliwa pale bandarini. Mimi atakae zuia madawa haya niambieni ili nijue chombo gani cha serikali, niambieni tu huyo aliyezuia nione ili na mimi nimzuie yeye moja kwa moja kuna mambo mengine ni rahisi sana wala msilalamike bali mwambie Waziri au Katibu Mkuu"alisema Rais Magufuli 
    Magufuli aliendelea kuweka wazi kuwa watu ambao wanakwamisha na kuchelewesha dawa kutoka ni watu ambao pia wanatoka katika wizara hiyo hiyo wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. 
    "Hata aliyempa nguvu ya kuzuia dawa wapo chini ya wizara yenu yaani ni nyinyi wenyewe, basi nyinyi vilaza sasa mtu yupo chini yenu, yaani mtu anayezuia yupo kwako anayezuiliwa yupo kwako bado mnakaa mnaimba nini. Mimi nataka haya niyashughulikie unajua mambo mengine mnakwamishana nyinyi wenyewe kama ni TRA mwambie Katibu Mkuu, mwambie Waziri wa Afya, mwambie Waziri wa Fedha tufike mahali tusikwamishane, kwa sababu anaweza akawa amekwamisha madawa yenu lakini madawa ya mtu binafsi anayaruhusu siku hiyo hiyo sasa hili ni lenu wala halihitaji kufika kwangu"alisisitiza Magufuli

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI