• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 16 March 2018

    Majaliwa awageukia wasomi, atoa ushauri

    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ni muhimu mfumo wa ufundishwaji wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini ukaboreshwa ili wanapomaliza waweze kujiajiri.
    Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. William Anangisye, ofisini kwake mjini Dodoma.
    Amesema wanafunzi hao wanapomaliza wanatarajiwa wawe na uwezo wa kubuni mbinu mbalimbali za kujiajiri na kuondokana na mtazao wa kusubiri ajira za kuajiriwa maofisini.
    "Kumekuwa na tatizo kubwa la wasomi wetu kuwa na mtazamo kwamba wanapomaliza masomo yao lazima waajiriwe. Upo umuhimu wa kubadili mtazamo huo kwa kuwapa mbinu zitakazowawezesha kujiajiri," amesema.
    Waziri Mkuu amesema wasomi hao wanaweza kuchukua kauli mbiu ya Rais Dkt. John Magufuli ya uchumi wa viwanda kwa kuanzisha kilimo cha mazao mbalimbali yatakayotoa malighafi za viwandani.
    Pia Waziri Mkuu amesema wasomi hao wanaweza kujikita katika shughuli za uchimbaji wa madini au usindikaji wa mazao mbalimbali, hivyo tayari watakuwa wamejiajiri kwa sababu ajira si za ofisini pekee.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI