Watanzania wametakiwa kuwa na ushirikiano katika kuhakikisha
wanatokomeza ugonjwa wa kifua kikuu ambao umeonekana sio rafiki kutokana na kugharimu maisha ya watu.
Akizungumza
katika maadhimisho ya Ugonjwa wa Kifua kikuu katika Manispaa ya Ilala,
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema amesema kuwa ugonjwa
huo unapaswa kupigwa vita na kila mtu.
Mhe.
Mjema ambaye ni mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, amesema kuwa ni
vema kila mtu anamlinde mwezake jambo ambalo litasaidia kupunguza idadi
ya wagonjwa wa kifua kikuu hapa nchini.
"
Wilaya ya Ilala sasa inatakiwa kuanzisha kampeni ya kutokomeza ugonjwa
wa kifua kikuu kwenda kwa mtu mwengine" amesema Mhe.Mjema.
Ameeleza
kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitema mate hovyo, bila kujua
kufanya hivyo kunaweza kuchochea ongezeko la ugonjwa wa kifua kikuu
kutokana ugonjwa huo unaambukiza kwa njia ya hewa.
"Imefika
wakati kupiga vita vitendo hatarishi kwa afya ikiwemo kuuza vyakula
pamoja matunda ambayo hayajaifadhiwa sehemu salama ili kuepuka
magonjwa" amesema Mhe. Mjema.
Mganga
Mkuu wa Ilala amebainisha kuwa kwa
mujibu wa shirika la afya duniani, Tanzania inashika nafasi ya sita kuwa
watu wenye ugonjwa wa kifua kikuu, huku Afrika ikiwa nafasi ya nne.
Ameseme kuwa katika Wilaya ya Ilala kuna maeneo ambayo
yanaongoza kuwa na wagonjwa wengi wa kifua kikuu ambayo ni Kata ya Buguruni, Ukonga, Kiwalani pamoja na Vingunguti.
Imeelezwa kuwa kata hizo zinachangia asilimia 80 kwa wagonjwa wenye kifua kikuu ambao wanagundulika takribani 5,000 kila mwaka.
Manispaa
ya Ilala wameadhimisha leo siku ya wagonjwa wa kifua kikuu katika kata
ya Mchikichini jijini Dar es Salaam wakiwa na kauli
mbiu ya mwaka huu ‘Viongozi tuwe mstali wa mbele kuongoza mapambano ya
kutokomeza kifua kikuu’.
No comments:
Post a Comment