Na. Apolonia kisite
Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation,limeingia makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara na kampuni ya simu za mkononi TIGO Tanzania yatakayowezesha wateja wa taasisi hizo kubadilishana fedha na huduma za fedha mtandao kupitia simu zao za mkononi.
Akizungumza katika hafla ya kutangaza ushirikiano huo,Mkuu wa Huduma za TTCL PESA Bw. Moses Alphonce amesema TTCL PESA inaona furaha kushirikiana na TIGO PESA katika kuwapa wananchi suluhisho sahihi la mahitaji yao ya fedha mtandao ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano za kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
Aidha amesema TTCL PESA imeazimia kuwapa wananchi huduma za kiwango cha juu kabisa cha ubora na unafuu wa gharama za kutuma,kupokea na kufanya miamala kwa kutumia simu zao.
Pia Bw. Alphonse amesema wamedhamiria kubadili mifumo ya malipo yote ya umma na binafsi,yasifanyike kupitia mtandao ili kuongeza usalama na ufanisi wa shughuli za ki uchumi na kijamii.
"wamejidhatiti katika kutoa huduma kwa haraka na usalama wa hali ya juu wa fedha za wateja wetu na tutafanya kila liwezekanalo ili wateja wetu wapate thamani halisi ya fedha zao kupitia viwango vya huduma zao" amesema Alphonse
Hatua hii ni mwendelezo wa jitihada za shirika la Mawasiliano Tanzania kurejea kwa kishindo katika soko la huduma za mawasiliano nchini Tanzania,hadi sasa TTCL imefanikiwa kufikisha huduma za 4G LTE katika mikoa 16 ya Tanzania bara na visiwa vya Pemba na Unguja.
TTCL imeendelea kuwa mhimili Mkuu wa mawasiliano nchini Tanzania ikiwa inaongoza kwa kutoa huduma ya Data Kwa taasisi za umma na binafsi sambamba na huduma za simu za mezani na simu za viganjani.
..
Wednesday, 21 March 2018
Habari
No comments:
Post a Comment