• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 16 March 2018

    Wananchi watakiwa kuelimishwa juu ya uwekezaji wa fedha

    Wananchi bado wanakabiliwa na changamoto ya uelewa mdogo wa masuala ya fedha hususani,kutambua faida na hasara za uwekezaji kwenye masoko ya mitaji na dhamana kwasababu bado wanahofu ya kuwekeza kwenye hisa kwa kuogopa kupata hasara.

    Ameyasema hayo Naibu katibu mkuu,wizara ya fedha na mipango Bi.Amina Shaaban ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa uorodheshaji wa hisa za TCCIA INVESTMENT PLC kwenye soko la hisa la Dar es salaam.

    Amesema changamoto hiyo inapaswa kutumika kama fursa kwao kwa kutafuta namna bora ya kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kubuni njia rahisi zitakazowezesha wananchi wengi kujiunga kwenye huduma hizo.

    Pia amesema serikali inatambua kuwa sekta binafsi kwa ujumla wake ni muhimu katika ukuzaji na uendelezaji wa uchumi wa taifa,hususani uchumi wa viwanda.

    Sambamba na hayo Bi.Amina ametoa wito kwa mwenyekiti pamoja na bodi yake kujiwekea utaratibu wa kufanya mkutano mkuu wa wanahisa kila mwaka pamoja na kujadili taarifa za shughuli za kampuni na kuandaa mipango endelevu ya utoaji wa elimu ya masuala ya hisa kwa wanahisa.

    Kampuni ya hiyo ilianzishwa na chama cha wafanyabiashara  wenye viwanda na kilimo ikiwa na dhumuni la kutoa fursa kwa wanachama wake kuunganisha akiba zao ili kuwawezesha kuwekeza na kumiliki uchumi kwa pamoja.

    Kwa upande wa Afisa mtendaji mkuu TCCIA Investment PLC Donald S.Kamori amesema zipo changamoto mbalimbali zinazokabili uwekezaji lakini ipo moja ambayo wao wanaona inaathiri ukuaji wa mitaji inayohitajika sana katika uwekezaji.

    "Changamoto hiyo inahusu uelewa mdogo wa masuala ya uwekezaji kwa njia ya hisa,inaonekana watu wengi hawaelewi faida za hisa na njia za kujikinga na athari zinazoweza kutokea"amesema Donald.

    Pia amesema changamoto hiyo inakuwa kubwa zaidi pale inapohusu uwekezaji wa pamoja,kwani watu wenye kipato cha chini wanaona hawana uwezo wa kuwekeza hivyo wao wanaamini kuwa wakiunganisha amana zao wanaweza kufanya mambo makubwa na yenye faida.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI