• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 15 March 2018

    USHIRIKA WAMPATIA RC MAKONDA TANI 120 ZA SARUJI KWAAJILI YA UJENZI OFISI ZA WALIMU DAR

    Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amepokea Tani 120 za Saruji ambazo ni sawa na Mifuko 2,400 ya saruji kutoka kwa Vyama vya ushirika 27 vya Mkoa huo vilivyoguswa na kempeni ya Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu Dar es salaam.

    Mifuko hiyo 2,400 ina uwezo wa kufyatua Tofali 70,000 ambazo zitejenga ofisi 14 za kisasa kwaajili ya Walimu.

    Akipokea mifuko hiyo RC Makonda amesema shughuli ya ujenzi wa ofisi za walimu inaendelea vizuri  ambapo amewashukuru wadau wote wanaoendelea kuchangia kampeni hiyo inayolenga kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu ili waweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi na mwisho wa siku tuwe na wataalamu wa kutosha.

    Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika  Dar es salaam Bwana Tumaini Wilfred amesema wameguswa Sana na jitiada zinazofanywa na RC Makonda kwenye kuboresha mazingira ya walimu ndio maana wameona na hao Kama ushirika wasibaki Nyuma  jambo hilo jema linalolenga kuleta ukombozi wa fikra.

    Aidha Bwana Tumaini amesema Ushirika utaendelea kuunga mkono kwa kila hali juhudi zinazifanywa na RC Makonda.

    KWA PAMOJA TUBORESHE MAZINGIRA YA ELIMU DAR ES SALAAM.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI