Wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto imewataka waganga wa tiba za asili kuondoa mabango yote yaliyobandikwa kwenye maeneo mbalimbali ambayo yanayoonesha aina za magonjwa ambayo wanayatibia kwani hairuhusiwi kisheria.
Ameyasema hayo Naibu waziri wa afya, maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati akitoa tamko kuhusu usajili wa waganga wa tiba za asili katika ofisi za wizara hiyo na kuwataka mabango hayo yaandikwe jina la mganga,sehemu anayopatikana na mawasiliano .
Aidha amelitaka baraza la tiba za asili na mbadala likamate vyombo vya habari na wale wote wanaotoa matangazo na vipeperushi vya tiba za asili katika magari na maeneo mengine bila kibali maalum.
Sambamba na hayo amesema ni lazima kila mganga wa tiba za asili asajiliwe,kusajili vituo vyao,wasaidizi wao pamoja na dawa serikalini kupitia baraza la tiba za asili na mbadala fomu zinapatikana katika ofisi ya Mganga mkuu wa halmashauri bure haziuzwi,hivyo waganga na taasisi nyingine yeyote hazijapewa majukumu ya usajili.
pia amesema hadi tarehe 31 Desemba 2017 baraza la tiba za asili na mbadala wasajili waganga 16,300,vituo 212 na dawa za asili 5.
Aidha amesema serikali inawahamasisha waganga wa tiba za asili kujiepusha na mgongano katika jamii kwa kutohusisha ushirikina na uchawi kama chanzo cha ugonjwa.
"waganga shirikianeni katika kupanga mikakati ya kudhibiti na kuondoa kabisa vitendo vibaya vinavyochafua taaluma yenu mfano upigaji ramli,mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi,ukeketaji na vitendo vyote vinavyohusishwa na uchawi na ushirikina"amesema Dkt.Ndugulile.
Amesema waganga wote waliosajiliwa na watakao jisajili kubandika vyeti vyao vya usajili katika vituo vyao vya tiba.
Vilevile wamebaini baadhi ya watumishi wa serikali wasio waadilifu wanaoshirikiana na viongozi wa vyama vya waganga wa tiba za asili kwa kuwatisha waganga kwamba watawafunga iwapo watashindwa kutoa fedha wanazohitaji na wakati mwingine huwaweka rumande.
Hivyo ametoa wito Kwa ofisi za serikali na halmashauri kushirikiana kwa pamoja katika kutatu makosa hayo.
No comments:
Post a Comment