Akizungumza na waandishi wa habari Dkt.Ndugulile amesema lengo kuu la maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa na kujenga ufahamu wa wananchi juu ya ugonjwa huo hatar wa shinikizo la macho,katika azma nzima ya kuzuia ulemavu wa kutoona.
Amesema Tanzania inakadiriwa kuwa na watu 1,740,000 wanamatatizo ya kutokuona vizuri kunakosababishwa na matatizo yoyote yakiwemo mtoto wa jicho,tatizo la upeo mdogo wa macho kuona ikifuatiwa na shinikizo la macho.
Aidha Dokt. Ndugulile amesema kuna umuhimu mkubwa sana wa kupima macho angalau mara moja kwa kila mwaka kwani ugonjwa huo husababisha upofu kwa taratibu sana kwa siku hadi siku bila dalili yoyote katika hatua ya awali.
" Maadhimisho hayo yanabeba kauli mbiu isemayo "OKOA UONI WA MACHO YAKO" ikiambatana na ujumbe mahususi kwa jamii na wadau wa huduma za macho na afya kwa ujumla "NENDA KAPIME IWAPO UNASHINIKIZO LA MACHO".amesema Dkt.Ndugulile.
Pia ugonjwa huo wa shinikizo la macho mara nyingi hujitokeza kuanzia umri wa miaka ya 40 na kuendelea kuzidi kadri umri wa kuishi unapozidi kuwa mkubwa.
Sambamba na hayo Dkt.Ndugulile amesemaAhmed serikali kwa kushirikiana na wadau wanaendelea kuboresha miundo mbinu pamoja na kuongeza wataalamu wa afya ya macho,vifaa tiba ili kusogeza huduma za uchunguzi na tiba kwa matatizo ya macho ikiwemo shinikizo la macho karibu zaidi na wananchi ili kupunguza umbali wa kufuata huduma ya macho, pia watahakikisha hali ya upatikanaji wa dawa za macho katika vituo vya tiba inazidi kuimarika.
No comments:
Post a Comment