• Breaking News

    ..

    ..

    Monday 9 April 2018

    "Asilimia 70 ya maeneo ya pembezoni mwa bahari Kigamboni hayajaendelezwa"

    Wananchi wa wilaya ya Kigamboni wametakiwa kutambua KDA imefutwa badala yake kazi zote za KDA zimekasiniwa kwa halmashauri ya manispaa ya Kigamboni hivyo wananchi walio na vibali wanaweza kuyaendeleza maeneo yao Kwa kufuata ramani za mipango miji.

    Ameyasema hayo Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Hashim Mgandilwa wakati akitoa taarifa ya zoezi la kuondoa uhalifu  sehemu za fukwe za bahari lililofanyika wiki iliyopita ndani ya siku sita.

    Amesema dhamira ya zoezi hilo ni kuimarisha ulinzi maeneo ya fukwe,kuwajua wamiliki wa viwanja vinavyotazamana na fukwe za bahari na kuangalia miundombinu na majengo yaliyojengwa ndani ya mita 60 kutoka baharini.

    Aidha amesema katika zoezi hilo wamebaini asilimia 70 ya maeneo ya fukwe bado hayajaendelezwa,wamiliki wa maeneo hayo ya fukwe bado wanadhana ya kuamini KDA ipo inawazuia kujenga katika maeneo yao,ujenzi holela bado unaendelea katika maeneo hayo na wananchi wengi hawazingatii ramani za mipango miji.

    Pia Mgandilwa amewataka wamiliki wote wa viwanja vilivyokaribu na fukwe za bahari watambue sehemu hizo ni za uwekezaji na siyo kwaajili ya makazi ya kuishi.

    Ameongezea kwa kusema kwa waliojenga ndani ya mita 60 kutokea baharini hairuhusiwi mpaka upate kibali na vibali vinatolewa ndani ya siku tano.

    Kwa upande wa afisa mipango miji manispaa ya Kigamboni Nice Mwakalinga amesema wanapata changamoto kubwa katika utoaji wa vibali vya ujenzi katika maeneo ambayo hayajapimwa,wananchhi wengi siyo waaminifu kwa kutaka vibali katika maeneo yasiyo yao na baadhi ya wananchi wanachelewa kupata vibali kutokana na kutokukamilisha nyaraka zinazohitajika.

    Pia bi.Mwakalinga amesema vibali hivyo lazima vigharamiwe kwasababu ya taratibu nyingi ambazo wanapitia hivyo lazima zigharamiwe katika kila kibali kinachotolewa. 

    Pia kwa upande wa Diwani Kata ya Kigamboni na ni Mwenyekiti wa uwekezaji manispaa ya Kigamboni Dotto Msawa amewaomba wawekezaji wajitokeze kuwekeza katika manispaa hiyo na kuwataka wananchi waliojenga ukuta Kwa ukuta katika fukwe wavunje na kuacha mita tatu.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI