• Breaking News

    ..

    ..

    Monday 9 April 2018

    Mfumuko wa bei wa taifa umepungua kufikia asilimia 3.9 Kwa mwezi march

    Na Stahmil Mohamed
    Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi marchi 2018 umepungua hadi kufikia asilimia 3.9 ikilinganishwa na mwezi ulioisha.

    Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa sensa na takwimu za jamii  Bw Ephraim Kwesigabo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mfumuko wa bei kwa mwezi march ambapo amesema kuwa mfumuko wa bei wa Taifa kwan mwezi march2018 umepungua hadi kufikia asilimia 3.9%ikilinganishwa na asilimia 4.1%ilivyokuwa mwezi februari.

    Aidha Kwesigabo amesema kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwezi ulioisha kumechangiwa na mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na baadhi ya bidhaa hizo za vyakula ni mtama kwa asilimia7.1unga wa mihogo kwa asilimia 6.7maharage kwa asilimia 3.9 mihogo mibichi kwa asilimia16.6 na ndizi za kupika kwa asilimia16.7

    Hata hivyo kwesigabo amesema hali ya mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki haijapishana sana na Tanzania ambapo nchi ya Uganda mfumuko wa bei kwa mwezi march 2018 umepungua hadi asilimia 2.0 kutoka asilimia 2.1 kwa mwezi februari 2018na kwa upande wa Kenya mfumuko wa bei kwa mwezi march2018 umepungua hadi asilimia 4.18 kutoka 4.46 kwa mwezi februari2018.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI