• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday 21 April 2018

    Mjane adondosha chozi

    Mtu mmoja Mkazi wa Mnazimmoja barabara ya Sukuma  na Mafya   jijini Dar es Salaam anayefahamika kwa jina la Wechu Salumu Abdallah amemlili Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Paul Makonda amsaidie kwani amedhulumiwa nyumba na kupigwa mnada .
    Akizungumza na waandishi wa habari Bi. UWechu Abdallah amesema anamwomba mkuu wa mkoa asikie kilio chake kwani amedhulumiwa nyumba ambayo ni ya urithi,waliyoaachiwa ambapo wapo ndugu wanne wanayomiliki nyumba hiyo.

    Amesema nyumba hiyo ya Urithi amezelumiwa na MTU anayefahamika kwa jina la Mushi Mtakwa mwenye kampuni inayotambulika MOSAM COMPANY ambaye alikubaliana naye kujenga ghoropha 8 ambazo wangegawana lakini baadae wamegeuka na kuchukua nyumba hiyo na kuipiga mnada ambapo ametakiwa kuweka zuio kwa siku 14 tu.

    "Mkuu wa mkoa naomba unisaidie Mimi mnyonge kwani nimeachiwa watoto nawahudumia hakuna anayenisaidia mlnyumba hii ndio ulikuwa msaada wangu sasa hivi Niko nje sina msaada hivyo nakuomba mkuu  wangu unisaidie nipate haki" Amesema

    Ameeleza kuwa yeye pamoja na ndugu zake hao walioachiwa nyumba hiyo walikubali kuwa mjenzi huyo ajenge ghorofa izo 8 ambapo wangegawana 4 kwa 4 na kufuatia makubaliano hayo walifuata misingi yote ya sheria na wakaandikishana kwa makubaliano ya kujenga ghorofa.

    Amendelea kusema mmoja wa mrithi wa Mali hizo aliamua kuondoka kwenye mkataba na kutaka apewe gawio la fedha zake ambazo ni takribani ya shilingi Milioni 70 na laki 6 ambapo walimweleza mjenzi wao na kukubali kumpatika kasi hicho cha fedha wakaandikishiana na wakampatia kiasi cha fedha hizo lakini Dada yao Huyo alitaka kuongezewa.

    Amesema wamwambia kuwa anataka kuongezewa hivyo wakaenda mahakamani na kuhakikisha wakafanya makubaliano ambapo mjenzi huyo aliwapatia fedha hizo na kumpatia Dada yao,na baada ya hapo walitakiwa kumwondoa katika makubaliano.

    Aidha mama huyu amemwomba RC Makonda kumsaidia kwani nyumba hiyo tayari imeuzwa na mnada ulifanyika bila ya matangazo yoyote na wakati kesi bado uko mahakamani.

    Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa amesema ni kweli nyumba hiyo imepigwa mnada na watu waliofika kuleta tangazo ofisini kwake na kupigwa mnada pasipokuwa na matangazo kwa wananchi wa mtaa huo kuwa nyumba inauzwa .

    Nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa Sukuma Kariakoo Ilala jijini Dar es Salaam ilipigwa mnada na kuuzwa kwa thamani ya shilingi milioni 350 ambapo walifanya mnada bila ya kumshirikishwa Msimamizi wa Mirathi hiyo.


    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI