• Breaking News

    ..

    ..

    Monday 23 April 2018

    Wadau na taasisi binafsi zimeombwa kusaidia wanaosomea fani ya utalii ili kukuza utalii nchini

    Wizara ya Maliasili na Utalii Wakishirikiana na chuo Taifa cha Utalii(NCT)Wamewaomba wadau wa maendeleo,taasisi binafsi kuendelea kuwasaidia wanafunzi wanaosomea fani ya ukarimu na utalii ili kusaidia sekta ya utalii kukua Nchini.

    Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam Kaim Mkurugenzi wa Mafunzo na shughuli za kitaaluma STEPHEN MADENGE amesema kwa kuzingatia soko la ukuaji wa sekta ya Utalii na Ajira za Utalii Nchini Wanafunzi wanaosomea somo la Ukarimu kufanya tafiti mbalimbali ili kukuza ujuzi wao.

    Kwa upande Mratibuwa tamasha la career day EUNICE ULOMI amesema Watanzania wanatakiwa kupenda Utalii wao wenyewe na kuwafundisha Wanafunzi fani mbalimbali za utalii ili kukuza Utalii Nchini.

    Chuo cha utalii Nchini kimeandaa tamasha la Aprili27Mwaka huu kuanzia saa tatu asubuhi ambapo mgeni rasmi atakuwa katibu Mkuu Wisara ya Maliasili na Utalii

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI