Kamati ya maandalizi ya uhuru wa vyombo vya habari duniani (WPFD) inatarajia kuadhimisha miaka25 ya uhuru wa vyombo vya habari kwa hapa Tanzania itakayofanyika jijini Dodoma tarehe 2 na 3 mwezi ujao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwenyekiti taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Africa -Misa Tan Salome kusimari amesema katika maadhimisho hayo mgeni rasmi atakuwa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania dkt John Magufuli pia na wageni takribani 500 wakiwemo wadau mbalimbali wa vyombo vya habari watahudhuria hafla hiyo.
Amesema pia siku hizo mbili wataongelea mada mbalimbali ikiwemo haki ya kupata taarifa,wataangalia usawa wa kijinsia na changamoto zake,utendaji kazi wa vyombo vya habari vya mitandaoni na maonesho mbalimbali kutoka vyombo tofauti tofauti.
Aidha amesema kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho hayo ni " WAJIBU WA SERIKALI,VYOMBO VYA HABARI , HAKI NA UTAWALA BORA WA SHERIA.
"Kauli mbio hiyo imerejerea umuhimu wa kuwa na mazingira bora ya kuwa na vyombo vya habari na kusisitiza umuhimu wa vyombo vya habari na Sheria" amesema Kisumari.
Pia amesema kauli mbiu hiyo inawakumbusha waandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao kwa kuandika habari kwa usahihi na zenye ukweli.
Kwa upande wa makamu wa raisi umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania Jane Mihanji amesema kazi yao kubwa ni kuwaunganisha waandishi wa habari nchini kuwa pamoja na kuwapa mafunzo ya kitaaluma pamoja na vitendea kazi.
Pia Mihanji amesema katika maadhimisho hayo kufuatiwa na kauli mbiu yake wamejipanga kuwakumbusha waandishi wa habari wajibu wao kama wanataaluma na wanaiomba serikali iwajibike kwa kufanya kazi zao vizuri.
Aidha kwa upande wa Fausta Musokwa ametoa wito kwa washiriki wote siku ya maadhimisho kujitathimini wamefika wapi kwenye kuimarisha na kuwa na tasnia ya habari iliyokuwa imara na yenye uhuru.
Pia amesema wameweka msisitizo kwenye umuhimu kwa waandishi wa habari kulindwa na kuweza kufanya kazi kwa uhuru na nafasi ya kuandika habari.
No comments:
Post a Comment