• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday 25 April 2018

    Wakulima wametakiwa kuwa na viwango bora vya mazao ya nafaka

    Washiriki na wadau wa kilimo cha mazao ya nafaka wametakiwa kuzingatia viwango bora vya mazao ya nafaka na kuvipa kipaumbele ili kuweza kupata mazao zaidi na soko zuri.

    Ameyasema hayo Mkurugenzi mtendaji baraza la nafaka Eastern African Grain Council(EAGC) Gerlad Masika wakati wa kikao na wadau wa kilimo cha mazao ya nafaka ambacho kinaangalia upatikanaji wa masoko ya mazao ya nafaka kuwa mengi.

    Amesema lengo la  baraza la nafaka ni kuhakikisha biashara ya mazao ya nafaka inatendeka vizuri sokoni.

    Pia amesema jukumu la baraza hilo ni kuhakikisha mkulima akishalima na kuvuna mazao yake ayaweke kwenye viwango vinavyohitajika vyenye ubora na kumwezesha kupata soko.

    "Tutaweza kupata mauzo yaliyobora zaidi endapo tukiwa na viwango bora vya mazao ya nafaka vilivyowekwa na baraza la nafaka"amesema Masika.

    Aidha amesema baraza hilo la nafaka lina kazi nyingi zikiwemo kutoa taarifa ya masoko katika nchi za Africa mashariki,kuwaunganisha wadau wa kilimo ili waweze kufanya kazi kwa pamoja na kutoa mafunzo ya kilimo katika vyuo vyao.

    Kwa upande wa Mkurugenzi wa taasisi ya RUDI TANZANIA bw.Lameck Kikoka amesema kinachowafanya wakulima wengi wa Tanzania kutofikia viwango vyenye ubora wa mazao kwasababu hakuna ushawishi utakaomfanya mkulima aweze kuwa bora zaidi kwasababu bei ni moja hata kama zao likiwa na ubora au kukosa ubora.

    Aidha amesema wakulima wanatakiwa kupata elimu ya kutosha ili waweze kuwa na viwango bora vya mazao ya nafaka ili iweze kuwapa bei nzuri sokoni.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI