• Breaking News

    ..

    ..

    Friday 27 April 2018

    Asilimia 17.5 ya pato taifa inachangiwa na sekta ya utalii

    Imeelezwa  Sekta ya utalii imekuwa ikikuwa mwaka hadi mwaka na kuvutia zaidi ya watalii milioni moja na laki mbili(1,200,000)na kuchangia asilimia 17.5 ya pato la uchumi wa Taifa kwa mwaka.

    Ameyasema hayo Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya utalii ya taifa Devotha Mdachi wakati wa tamasha la Taaluma (career day) katika chuo cha taifa cha utalii Dar es salaam iliyoambana na mbalimbali yaliyoandaliwa na wanafunzi wa Chuo hiko.

    Amesema idadi ya watalii inaendelea kuongezeka na matarajio ya watalii kutoka katika sehemu mbalimbali zinazotoa huduma zinatakiwa kukidhi viwango vya kimataifa ili kufanya sekta hiyo kuwa na uhitaji wa watumishi wenye elimu,weledi na ujuzi stahiki.

    Pia Mdachi amesema Vijana wengi wajitokeze kuwania fursa za Utalii na Ukarimu itasaidia kupunguza tatizo la Ukosefu wa ajira,kuongeza kipato kwa vijana na kuinua Uchumi wa Nchi na kuondoa umasikini.

     Kwa upande wa mwenyekiti wa Bodi ya ushauri chuo cha taifa cha Utalii Benardetha  Ndunguru amesema chuo cha Utalii miongonimni mwa vyuo vilivyo mstari wa mbele katika kuhakikisha sera za nchi kwa kujenga nchi ya viwanda na kufikia uchumi wa kati inatekelezeka.

    Kaulima tamasha hilo limebebwa na Kauli mbinu isemayo "FURSA ZA AJIRA KWA VIJANA KUPITIA TAALUMA YA UKALIMU NA UTALII"  wakiwa na lengo la kufahamisha umma juu ya mafunzo na huduma mbalimbali zitolewazo na chuo hiko pamoja na fursa nyingine zitolewazo katika tasnia ya ukarimu na Utalii.

    Pia bi.Ndunguru amesema siku hii imelenga kuwaunganisha wadau wa sekta ya utalii na ukarimu pamoja na wanafunzi ambao watatarajia kuajiriwa na wadau tofauti tofauti mara wamalizapo masomo.

    Aidha kwa upande wa kaimu afisa mtendaji mkuu wa chuo cha taifa cha utalii SHOGO SEDOYEKA amesema Tamasha hilo LA Taaluma litasaidia wanafunzi kukuza ujuzi walioupata na kujiajiri wenyewe .


    Pia amesema Chuo cha Utalii ni miongoni mwa vyuo vilivyo mstari wa mbele katika kuhakikisha Sera za Nchi kwa kujenga Nchi ya Uchumi wa Viwanda inatekelezeka.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI