• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 3 May 2018

    Shirika la Posta limejipanga kufanya shughuli zake pasipo kutegemea mikopo

     Na Apolonia Kisite
    Shirika la posta Tanzania limejipanga kufanya shughuli zake pasipo kutegemea kuomba mikopo ili kujiendesha badala yake kutumia rasilimali walizonazo ili kuwasaidia kuwahudumia wananchi kuwapatia huduma bora.
    Ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam mwenyekiti wa Bodi ya posta Harun kondo wakati wa utoaji taarifa fupi juu ya utendaji wa shirika la posta Tanzania kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016 na 2017.


    Amesema kuwa licha ya changamoto walizopitia ikiwemo tatizo la nidhamu Kwa watenda kazi wizi wa mafuta jitihada zilifanyika Kwa kufanya mabadiliko Kwa watenda kazi ili kuhakikisha shirika la posta linapata faida badala ya hasara.


    Pia amesema katika kuhakikisha shirika la posta linaendana na serikali ya uchumu wa viwanda ofisi imeongeza vitendea kazi kama vile pikipiki magari ili kuhakikisha huduma ya posta inaenda mbali hadi nchi za nje na kujulikana kimataifa.

    Aidha amesema katika kuleta tija na ufanisi kwenye shirika  bodi wamefanya mabadiliko mbalimbali ya kiuongozi ili kuliwezesha shirika kwenda na spidi na sera ya serikali ya awamu  ya tano ya Magufuli ya HAPA KAZI TU.

    "Mabadiliko hayo ni pamoja na kuondoa viongozi waliokuwepo na kuweka vijana ambao wataweza kufanya kazi kwa maono na muelekeo  wa shirika,kasi ya utendaji ili kuleta tija na ufanisi  utakaokidhi matarajio ya shirika tunayoyataka" amesema Kondo.


    Pia amesema Kwa juhudi za bodi na menejimenti kufanyika wamefanikiwa kurejeshewa madeni ya pensheni za wastaafu ambayo wamekuwa wakidai serikali jumla ya shilingi bilioni 3.9 ambayo ni pensheni za wastaafu wa shirika la posta na simu la afrika mashariki hivyo kufikia mwezi machi mwaka huu deni limefikia shilingi 4.7.


    Pia Kondo amesema katika kipindi cha mwaka 2015/2016 shirika lilipata hasara ya shilingi 3,490,031,800/=,2016/2017 walipata faida ya shilingi 1,014,548,869 baada ya kodi na kipindi cha mwezi julai hadi mwezi desemba 2017 shirika lilipata faida ya shilingi 1,375,797,682 baada ya kodi.

    kwa upande wa mkurugenzi wa Tanzania post corporation Hassan Mwang'ombe   amesema bodi mpya iliyoundwa imeweka mifumo mipya na mashine ili kuhakikisha wanazuia ubadhirifu unaotokea wa rasirimali katika shirika.



    Aidha Mwang'ombe amesema shirika limetumia milioni 224 ambayo inajumuisha net smart,utrack,IPS,IFS na PAYMASTER kwa ajili ya mifumo kwa mwaka katika kuhudumia ofisi zaidi ya ofisi 120 zilizounganishwa nchini kote na zaidi ya compyuta 1000.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI