Waziri wa mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh Augustine Mahiga amewata wafanyakazi waliopo chini ya Wizara yake wanaopelekwa balozi mbalimbali kuhakikisha sifa stahiki zinazingatiwa kulingana na mahitaji husika ya Nchi.
Ameyasema hayo hayo Jijini Dar es salaam katika katika Mkutano wa baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kuwa wafanyakazi kuondoa Uzembe mahali pa Kazi kwa kufanya kazi kwa bidii kwa manufaa ya Taifa.
Amesema kila mfanyakazi anatakiwa athamini kazi aliyonayo kwa kuwajibika ipasavyo ili kusaidia malengo yaliyowekwa na baraza hilo yanatekelezeka.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa ushirikiano wa Mambo na Ushirikiano was Afrika Mashariki Susan Kolimba amesema serikali inawashukuru wajumbe wa baraza kuonyesha ushirikiano licha ya changamoto zilizopo na kuwaasa waendelee kudumu katika mashirikiano mazuri kiutendaji.
No comments:
Post a Comment