Katika hali ambayo inayotafriwa kama kuwa juu ya sheria baadhi ya watu wa meendelea kukiuka matakwa ya kisheria katika kutekeleza baadhi ya mambo yanayo takiwa kutekelezwa kwa kufuata sheria, Familia moja imelalamika kudai kuwa nyumba yao imevunjwa kinyume cha sheria.
Nyumba hiyo namba 868 iko Upanga mtaa wa Mfaume.
Akizungumza na vyombo vya habari Msemaji wa familia hiyo Edith Max amemwamba Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Makonda kusaidia kupata haki yao amabayo inaonekana kuporwa kwa nguvu na taasisi ya Khoja Shia ambayo ili uziwa nyumba hiyo na Furaha Finance ambayo ilibadilika na kuitwa I and M Bank.
Akieleza mkasa huo amesema Familia yao ilikopa fedha TSh Milioni 30 katika bank hiyo na kudai kuwa walipotaka kulipa deni hilo walizungushwa na baadaye kambi wa kuwa Kuna riba imeongezeka kutoka milioni 30, hadi million 90, wakakubali kulipa lakini kila wakifuatilia kulipa tena wakaendelea kuzungushwa hadi deni likafikia Milion 120 tena wa likubali kulipa laki bank hiyo ili endelea tena kuwapa kaenda siku ya kulipa baadaye wakabaini kumbe Kuna udanganyifu ilifanywa kwa kugushiwa hati ya Mirathi na mtu asiyetambulika na Familia.
Amesema, Familia yenyewe ili fungua Mirathi yake tarehe 17 Januari katika Mahakama ya mwanzo Kinondoni na Msimamizi wa Mirathi hiyo Max Edmund Kafipa .
Awali anasema, suala hili walilipeleka kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Makonda katika Kampeni yake ya kuwa sikiliza walidhurumiwa nyumba, viwanja na Mashamba iliyofanyika mwezi January ambapo tarehe 30 pande zote ziliitwa na kujadilianakwa wanasheria na maamuzi yao yanatarajiwa kutolewa tarehe 7 May 2018.
Hata hivyo amesema kabla ya kuanza kuvunja nyumba hiyo wahusika waliopewa uzio la kuvunja lakini walikuwa na kuvunja nyumba hiyo Jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
"Wakili wao alitamka wazi kwa Makonda hana Mamlaka ya kuingilia mabo haya na hii nyumba tulikuwa tunaitaka muda mrefu" alisema
"Jana walituita wa kasema wanataka watulipe pesa wakatuuliza mnataka tuwape beigani ? tukasema tulipeni bilion 2 wa kasema wakajadiliene watatujulisha baadaye tukashangaa wakaja kuvunja nyumba yetu" Amesema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mfaume AbdulKarim Gulam Shambe amekili kuwepo kwa Sakata hilo na kwamba wakati wakati wa nakuja kuvunja nyumba hiyo walitoa taarifa wakati wamesha anza Kuvunja, na kueleza kuwa anafahamu suala hilo lilikuwa tayari mahakamani na baadaye kupelekwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
No comments:
Post a Comment