Na Apolonia kisite
Tanzania imeendelea kupanda hadi kufikia nafasi ya 7 kwa mwaka 2017 kati ya nchi 10 za bara la Afrika zenye ushawishi wa kuwavutia wawekezaji kuwekeza na kupelekea uchumi wa nchi kuzidi kukua siku hadi siku ambapo ikilinganishwa na mwaka 2014 Tanzania ilishika nafasi ya 11 na nafasi ya 9 Afrika Kwa mwaka 2016 kabla ya kupanda nafasi ya 7.
Ameyasema hayo Leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji Kituo cha Uwekezaji (TIC) Geoffrey Mwambe wakati akitoa taarifa kuhusu mafanikio ya kituo Kwa kipindi cha januari hadi Aprili 2018 amesema kituo katika kipindi husuka cha miezi kimefanikiwa kuandikisha miradi mipya 109 ambayo inatarajia kuwekeza mitaji ya kiasi cha dola za kimarekani milioni 13.3 na kuajiri wafanyakazi wapya 18,172.
Amesema Uwekezaji zaidi katika sekta za ujenzi,uzalishaji,uzalishaji viwandani,usafirishaji wa mizigo,kilimo na miundombinu katika miradi hiyo 28 sawa na 34.86% inamilikiwa na wageni, miradi 3 sawa na 2.75%ni ubia na miradi 68 sawa na 63.40% inamilikiwa na Watanzania.
Pia amesema kituo cha uwekezaji kimeshiriki makongamano ya biashara nje ya nchi,kupokea ujumbe wa wafanyabiashara na wawakilishi wa serikali kutoka nje,kuzungumza na mwekezaji mmoja mmoja na kuandaa makongamano ya kibiashara ndani ya nchi ili kuitangaza Tanzania ndani ya na nje ya nchi kama sehemu bora ya uwekezaji.
" Katika kipindi husika kituo kimeshiriki jumla ya makongamano matano ya biashara na uwekezaji katika nchi za Uholanzi,Korea kusini, Hispania,Kenya na Dubai na makongamano hayo yamevutia wawekezaji kuwekeza katika sekta za kilimo na uongezaji uthamani wa mazao ya kilimo,viwanda,nishati,ujenzi,utalii,miundombinu,tehama,afya,gesi na mafuta"amesema Mwambe.
Aidha Mwambe amesema kituo kimefanikiwa kupanua huduma zake kwa wananchi kwa kuongeza ofisi nne za kanda katika mikoa ya Dodoma,Dar es salaam,Mtwara na Kigoma ambazo Kanda ya kati (Dodoma,Morogoro na Singida) Kanda ya mashariki (Dar es salaam na Pwani)Kanda ya magharibi (Kigoma,Tabora,Katavi na Rukwa) na Kanda ya kusini (Mtwara,Lindi na Ruvuma.
Pia ametoa wito kwa wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya,wakurugenzi watendaji wa wilaya,miji,manispaa na majiji pamoja na watendaji wakuu wa taasisi zote za serikali kuongeza Kasi za uboreshaji wa huduma zao kwa wawekezaji.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uhamasishaji uwekezaji John Mnali amesema miundombinu kama umeme barabara ni changamoto kwa wawekezaji na serikali inaendelea kushughulikia ili kuboresha mazingira ya wawekezaji waendelee kuongezeka siku hadi siku.
Aidha amesema Serikali naendelea kupatia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazokuwa vikwazo kwa wawekezaji na inatioa utaratibu wa upatikaji wa Ardhi kwa wawekezaji
Kituo cha Uwekezaji kinaendelea kutoa ushirikiano kwa Taasisi n Mamlaka zote Nchini,kujenga uelewa,kutoa miongozi na kusimamia Ujenzi wa Viwanda Nchi nzima katika mikoa na Wilaya zote.
No comments:
Post a Comment