• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 8 May 2018

    Mfumuko wa bei wa taifa umepungua kufikia asilimia 3.8

    Na Apolonia kisite
    Mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Aprili,2018 umepungua hadi kufikia asilimia 3.8 ikilinganishwa na asilimia 3.9 ilivyokuwa mwezi machi 2018.


    Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi mkuu ofisi ya taifa ya takwimu Ephraim Kwesigabo amesema kupungua Kwa mfumuko wa bei imetokana na kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma Kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili,2018 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi machi,2018

    "kupungua Kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili,2018 kumechangiwa na kupungua kwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula"amesema Kwesigabo.

    Pia Kwesigabo amesema baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei kati ya Aprili,2017 na Aprili,2018 ni mafindo kwa asilimia 5.2,unga wa mahindi asilimia 5.6,mtama asilimia 7.3,unga wa mihogo asilimia 9.3,maharage asilimia 9.2 na mihogo mibichi asilimia 13.2.

    Hata hivyo amesema hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika mashariki haujapishana sana ikiwa Uganda kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili,2018 umepungua hadi asilimia 1.8 kutoka asilimia 2.0 kwa mwaka ulioishia mwezi Machi,2018, Kenya umepungua hadi asilimia 3.73 kutoka asilimia 4.18 kwa mwaka ulioishia mwezi machi,2018.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI