• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 9 May 2018

    RC MAKONDA ATOA ANGALIZO KWA WAKANDARASI "WAPIGAJI"


    Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaonya wakandarasi wenye tabia ya kutengeneza Barabara za chini ya kiwango na kuharibika ndani ya muda mfupi jambo linalosababisha hasara kwa serikali na usumbufu kwa watumiaji wa  vyombo vya usafiri.

    RC Makonda ametoa onyo hilo wakati wa hafla ya utiaji wa saini kwa Mikataba Nane ya mradi wa matengenezo ya Barabara, Mifereji ya Maji na Culvets inayotekelezwa na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini TARURA yenye tahamani ya zaidi ya Billion 5.8 .ambapo amewataka TARURA kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ujenzi wa barabara hizo.

    Aidha RC Makonda amezitaja Barabara zitakazojengwa kupitika mradi huo kuwa ni pamoja na Tegeta Nyuki, Msasani, Magomeni Makuti,Migombani, Kimara baruti, Kibanda cha Mkaa, Sheikh Bofu, Kwa Komba, Msigani, Sea clif na Mwananyamala Kisiwani.

    Hata hivyo RC Makonda ametoa wiki mbili  kwa TARURA kuhakikisha wakandarasi waliojenga barabara chini ya kiwango zinajengwa upya kwa gharama ya mkandarasi  ikiwemo barabara ya Mabatini ambapo barabara hizo zitakuwa na mifereji ya maji, sehemu za watembea kwa miguu na Taa za Barabarani.

    Pamoja na hayo RC Makonda amesema katika  uongozi wake hawezi kufumbia macho matumizi mabovu ya fedha za walipa kodi hivyo atahakikisha anasimama kidete kuhakikisha Dar es salaam inakuwa na barabara zenye ubora.

    Sanajari na hayo RC Makonda ametaka uwepo wa ushirikiano wa kikazi baina ya TARURA, TANROAD, TANESCO, DAWASCO na TTCL ilikupunguza ucheleweshaji wa miradi na ujenzi usiofuata taratibu unaopelekea uharibifu wa miundombinu.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI