wafanyabiashara wa Tanzania wanakumbana na changamoto ya uwezo wa kuzalisha bidhaa zenye viwango vya kimataifa.
Mkurugenzi wa Tan Trade tanzania Edwin Rutageruka amewashauri wafanyabiashara wote nchini kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora wa ili kuweza kuingia kwenye ushindani wa kuuza masoko ya kimataifa.
Ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam katika kongamano lililokutanisha wafanyabiashara wote nchini pamoja na ubalozi wa ufaransa katika kujadiliana namna ya kuwezesha bidhaa za kitanzania ziweze kusafirishwa na kuuzwa nchini ufarasa.
Pia Rutageruka amesema wafanyabiashara wa Tanzania kwa muda mrefu wamekuwa wanakumbana na changamoto hiyo ya kushindwa kuzalisha bidhaa zenye ubora hivyo kupelekea hata katika uuzaji wake katika masoko ya kimataifa bei wanayouza hailingani na soko huria lililopo.
kwa upande wa balozi wa Tanzania nchini ufaransa Samweli Shelukindo amesema wafanyabiashara wa Tanzania watumie fursa hizo za kufanyabiashara na waangalie ni bidhaa zipi zinaweza kusafirishwa na kuweza kuuzwa nchini ufaransa kwani wafaransa wanatafuta wafanyabiashara wa tanzania wenye nia ya kupeleka bidhaa nchini kwao.
Aidha kwa upande wake balozi wa ufaransa nchini Tanzania Frederiki Clavier amesema tanzania ni nchi yenye mandhari nzuri ya kufanya uzalishaji wa kilimo cha biashara hivyo watu watumie ardhi vizuri waliyo barikiwa na mungu katika kuzalisha ili kukuza uchumi wa nchi yao kuendana na kauli ya raisi Dkt.John pombe magufuri ya hapa kazi tu na Tanzania ya viwanda.
No comments:
Post a Comment