• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday 19 April 2018

    Hospitali ya mama na mtoto ya chanika yazinguliwa rasmi

    Rais wa Shirika la Misaada la Korea Kusini KOICA Bi.Lee Mi Kyung amezindua Hospital ya mama na mtoto Chanika iliyojengwa kwa jitihada binafsi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda alietafuta wafadhili hao.

    Ujenzi wa Hospital hiyo ya kisasa umegarimu zaidi Shillingi Billion 9.8 ambapo ndani kuna vyumba vya kisasa vya upasuaji, vyumba vya Madaktari, Maabara,Chumba cha Mionzi, wodi ya wazazi,wodi ya watoto njiti, Theater, vyumba vya kujifungulia, ICU, Vyoo vya kisasa pamoja na nyumba za familia 28 za madaktari ambapo ndani ya nyumba hizo kuna kila kitu.

    RC Makonda amesema aliamua kutafuta wafadhili wa kujenga Hospital hiyo baada ya kuona kilio cha kinamama waliokuwa wakipoteza maisha na watoto baada ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.

    Aidha RC Makonda amemuomba Rais wa KOICA kumjengea hospitali nyingine mbili kwenye Wilaya mpya za Ubungo na Kigamboni ili kusaidia maboresho ya huduma za afya.

    Pamoja na hayo RC Makonda ameshukuru serikali ya Korea kusini kwa ufadhili wa hospital hiyo yenye hadhi ya kimataifa.

    kwa upande wake Rais wa KOICA Bi. Lee Mi Kyung amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika masuala mbalimbali ya maendeleo huku akipongeza Tanzania kwa kudumisha amani tofauti na Mataifa mengine.

    Uzinduzi wa hospitali hiyo umeenda sambamba na uzinduzi wa magari mawili ya kisasa ya wagonjwa (ambulance).

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI