• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday 18 April 2018

    Kinababa walioitikia wito wa RC Makonda wakubali kulea watoto wao

    Idadi kubwa ya Kinababa walioitikia Wito wa kufika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda wamekubali kutoa matunzo ya mtoto huku wengi wao wakipongeza Zoezi hilo kwa kuweka mazingira bora kwa Mtoto.

    RC Makonda amesema hadi kufikia jana Kinababa waliokubali kutunza watoto walifikia 540 na kinababa 60 walipimwa DNA ambapo amewapongeza wenza wote waliofika na kukubali kuwatunza watoto ambapo ametangaza vita Kali kwa wale wanaume watakaokaidi wito wa serikali.

    Licha ya Leo kuingia siku ya nane tangu lilipoanza, bado idadi kubwa ya kinamama wapya wameendelea kujaa Ofisini kwa RC Makonda ambapo amesema kila aliefika kwake atahudumiwa.

    Hata hivyo RC Makonda amesema idadi ya wananchi waliofika ofisini kwake ni zaidi ya 17,000 ambapo idadi ya waliosikilizwa hadi kufikia Jana walikuwa Wananchi zaidi ya 5,024.

    Aidha RC Makonda amewaasa wenzi waliopatanishwa kuepuka kupandikiza chuki kwa watoto kwakuwa lengo la Zoezi hilo ni kuweka ustawi bora kwa familia.

    Nao baadhi ya kinababa wamesema kupitia Zoezi hilo la RC Makonda limewakumbusha kuwa kukirijukumu la kuwalea watoto na kukiri kuwa walikuwa wakifanya kosa kubwa kutelekeza familia.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI