• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday 18 April 2018

    Zaidi ya Kampuni 35 za kifaransa zinatafuta fursa za uwekezaji nchini

    Moja Kampuni ya ufaransa inatarajia kujenga kiwanda cha unga wa muhogo Lindi hapa nchini kitakachokuwa kinazalisha tani laki tano za unga wa muogo kila mwaka.

    Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji Charles Mwijage amesema limekuja kundi la wawekezaji wafaransa lenye zaidi ya makampuni 35 kutafuta fursa za uwekezaji na biashara hapa nchini.

    Amesema jitihada na maelekezo ya Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Magufuli ya kuwataka mabalozi wa Tanzania huko walipo kuhakikisha suala la uwekezaji na biashara linatiliwa umuhimu zimeanza kuleta matunda.

    Kwa upande wa mwenyekiti wa sekta binafsi Tanzania  (TPSF) Reginald Mengi amesema kukutana na wawekezaji hao kutoka ufaransa wamepata fursa kubwa katika kushirikiana nao katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya ujenzi na katika miradi mingine mikubwa ya standard gauge na kilimo.

    "Tanzania ina utajiri mkubwa sana lakini hauonekani,utajiri tulionao ikiwemo amani na utulivu kwani wenzetu wamekuwa wakivitafuta sana"amesema Mengi.

    Aidha Mengi ewataka watanzania wajiamini kama wanaweza na kuchangamkia fursa walizoleta wafaransa katika sekta mbalimbali hapa nchini.

    Pia kwa upande wa balozi wa Tanzania nchini ufaransa Samweli Shelukindo  amesema  wanatekeleza sera ya diplomasia ya uchumi na kuunga mkono juhudi za Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Magufuli katika kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI