Mitazamo ya wananchi kuhusu Elimu inayotolewa bure imebadilika kwa kiasi kikubwa kutokana na matokeo ya Wanafunzi kutokuwa mazuri kwa Watoto wao ambapo mwaka 2017,Wananchi 9 kati ya 10(87%) wanasema ni bora kuongeza viwango vya Elimu,hata kama italazimu kulipa ada ili kusaidia Watoto kupata Elimu bora kuliko bora elimu.
Matokeo hayo yametolewa na TWAWEZA katika Utafiti wake uitwao Elimu Bora au bora Elimu?matokeo hayo yanatokana na Takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahijiwa elfu moja miasaba themanini na sita(1,786)kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara(Zanzibari haihusuki kwenye utafiti huu)kati ya mwezi septemba na octoba mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza Aidan Eyakuze amesema Wazazi wachache sana huzingatia ada nafuu(6%) umbali wa shule(18%) na Wazazi wengi hupeleka Watoto wao shule kwa kuzingatia zaidi viwango vya juu ufaulu wa shule husika kwa asilimia 72 hali hiyi huonyesha jinsi wazazi wanataka elimu bora na wameonesha utayari wa kuigharamia.
Kwa upande wake Mdau wa Elimu Nderakindo Kessy amesema elimu imeingiliwa na siasa kwani wengi waliotoa hoja ya kuwa elimu Bure Watoto wao hawasomi katika shule ambazo elimu no bure kwa sababu huona ufalu wa Watoto wao hautakuwa wa kiwango kutokana na changamoto zinazozikabili hizo shule has a za serikali.
Kwa upande wake Mwalimu Dr Richard Shukia amesema katika shule nyingi elimu hutolewa bure kuna changamoto kwa waalimu kuwafundisha wanafunzi darasa moja wanafunzi wengi,vifaa vya kufundishia,hivyo kupelekea ufundishaji kuwa mgumu ili wanafunzi waelewe vizuri .
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa twaweza ametoa wito"ujumbe wa msingi wa wananchi kuhusu suala la elimu nchini ni huu wananchi wako tayari kuilipia Elimu bora kwa ajili ya Watoto wao.Mitazamo ya Wananchi inaonekana kubadilika kwa kiasi kukubwa katika kipindi Fulani,ikiashiria kuwa sasa wanaelewa kilichofanyika na walipoteza Utafiti huu unaridhisha kuwa wanapaswa kuwa sehemu muhimu ya mjadala wa kitaifa utakaolenga kuboresha matikeo ya Elimu yetu Nchini"
No comments:
Post a Comment