Wadau wa usafirishaji wa Abiria na Mizigo wameiomba serikali kupunguza tozo mbalimbali za kodi ambazo zimekuwa changamoto kubwa katika uendeshaji wa sekta hiyo.
Wakizungumza leo jijini Dar es salaam katika Semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa vyombo vya usafiri vya Majini na Nchi kavu (Sumatra )wadau hao wamedai kwamba serikali imekuwa ikitoza kodi mbalimbali ,wakitolea mfano kodi ya mafuta kwa kiwango kikubwa, hali ambayo inawafanya kushindwa kumudu gharama za uendeshaji wa Huduma za usafirishaji..
Akizungumza Mkurugenzi udhibiti usalama barabarani Johansen Kahatano amesema kwamba wamiliki na madereva wengi wamekuwa wakikiuka wajibu wao hivyo semina hiyo ina malengo ya kutoka elimu ya namna ya uendeshaji wa sekta ya usafiri kwa mujibu wa sheria
Mmoja wa Wadau hao Chuki Shaabani ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wamiliki wa Malori Wadogo na Wakati Nchini (TAMSTOA )amewambia wanahabari kuwa changamoto kubwa zinazowakumba ni kutozwa kodi kubwa,uharibifu wa miundo mbinu ya barabara, pamoja na kutungwa kwa sheria mbalimbali za usafirishaji bila kuwashirikisha wadau hao.
Kwa upande wake Mhadhiri Mstaafu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Thomas Mwaipopo ambaye alikuwa mwenyekiti wa semina hiyo, amesema kwamba baadhi ya wamiliki wa vyombo vya usafiri wamekuwa wakiajili madereva ambao hawana taaluma husika, hali ambayo inachangia kushindwa kubaini usalama wa magari wanapokuwa kazini na kusababisha ajari mbalimbali za barabarani.
Semina hiyo ya Wadau wa Usafirishaji wakiwemo Wamiliki na Madereva,imeendeshwa leo katika mikoa tofauti ya Dar es salaam,Mbeya ,Arusha na Mwanza baada ya Sumatra kubaini kuwa bado kuna chngamoto kubwa katika mifumo ya usafirishaji hususani usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi..
..
Friday, 18 May 2018
Home
Unlabelled
Wadau wa usafirishaji abiria na mizigo waiomba serikali kuwapunguzia tozo
No comments:
Post a Comment