• Breaking News

    ..

    ..

    Friday 18 May 2018

    RC MAKONDA AWAALIKA WANANCHI KUSHUHUDIA TUKIO LA RAIS MAGUFULI KUKABIDHI KOMBE KWA TIMU YA SIMBA

    Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewahakikishia usalama mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu watakaojitokeza kwenye Mechi Kati ya Timu ya Simba na Kagera Sugar itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Rais Dr. John Magufuli ambae atakabidhi kombe la Ubingwa wa VPL 2017/2018 kwa Timu ya Simba.

    RC Makonda amesema hayo wakati alipotembelewa ofisini kwake na viongozi wa timu ya Simba ambapo amesema kitendo cha Rais Magufuli kukubali kuwa mgeni rasmi usiku ya kesho ni heshima kubwa kwenye tasnia ya michezo kwakuwa uwepo wake utakuwa na manufaa makubwa katika maboresho kwenye sekta ya michezo.

    Aidha RC Makonda amesema anachofurahia ni kuona timu ya Simba iliyopo mkoa wa Dar es salaam inanyakua kombe jambo ambalo ni heshima kubwa pia kwa Mkoa.

    Kuhusu suala la msongamano wa magari  barabarani RC Makonda amesema watahakikisha hakuna foleni ili hata wale waliofungwa kwaajili ya Ramadhan waweze kuwahi nyumbani kufuturu ambapo ambapo amewasihi wananchi keza kwa Wingi.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI