• Breaking News

    ..

    ..

    Friday 18 May 2018

    Huyu ndeye Mshindi Wa Qur an tukukufu

    Mchujo wa mashindano ya kumpata mwakilishi atakae wakilisha kimataifa katika mashindano ya Quran yamefanyika leo katika Msikiti wa Kichangani uliopo magomeni Mikumi Jijini Dar es salaam.

    Akitoa shukrani zake mara baada ya kuibuka kidedea kijana Aboubakar Muhammed Omar amesema kuwa Shindano lililkuwa gumu kutokana alikuwa na akichuana na watunwenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi Quran ambapo amewaomba watanzania kuendelea kumuombea Dua kutokana yeye ndiye anaekwenda kuiwakilisha Nchi.

    Waumini Wa Kiislam wakisiliza QUR AN
    Aidha amewashukuru Majaji ,marafiki  pamoja na walimu wake kwa kumuombea Dua huku akisistiza waendelee kuwa nae begaa kwa bega wakati wote wa mashindano.

    Huyu ndie Mshindi Bw.Aboubakar Muhammed
    "Suala la kuwakilisha nchi ni zuri lakini linahitaji sana msaada wa Dua ili kuweza kufikia malengo"Amesema Aboubakar

    Kwa upande wake Mshiriki mwingine ajulikanae kwa jina la Ismail Ally Jumma kutoka Markaz ameeleza kuwa kilichompelekea kushindwa Shindano hilo ni kubadilika kwa sauti yake huku akidai ni Moja ya Changamoto za Swaum ambapo sauti yake ilibadilika ghafla kwa kukauka.

    Mashindano hayo yameshirikisha wanafunzi wanne kutoka katika Madrasa tofauti nchini.

    Michuano hiyo inatarajiwa kufanyika Tarehe 03-06-2018 katika ukumbi wa Diamond Jubilee upanga jijini Dar es salaam

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI