Mashindano Wiki ya Madhimisho ya elimu kwa shule za msingi yanayofanyika kila mwaka yenye lengo kuakisi kinachofanyika shuleni yamefikia kilele leo Mei 22 Manispaa ya Kinondoni jiji Dar es salaam.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Meya wa Manispaa hiyo Benjamini Sita amesema kuwa lengo ni kufikia ufaulu kwa asilimia 100 maana mwaka huu imekuwa tofauti kwani wameshindanishwa wanafunzi kielimu.
Hata hivyo Meya Wa Manispaa ya Kinondoni Ameahidi atahakikisha lengo hilo linafikiwa huku akiwapongeza walimu na wanafunzi ambao jitihada zao zinaonekana za kuinua elimu nchini ambapo kwasasa manispaa hiyo inaongoza kwa ufaulu nchini.
"Mashindano haya lengo ni kukuza sekta ya elimu kwani wanafunzi wanapata nafasi ya kushindana na kupata zawadi pia kuunganishwa na kuwa kitu kimoja .
Pia nawapongeza wanafunzi wote ambao leo wameshinda na kupata zawadi ambapo wataiwakilisha manispaa na wakishinda atawaandalia zawadi ambayo itakuwa chachu zaidi.
Kwa upande wake afisa elimu wa shule za msingi manispaa hiyo Kiduma Mageni amesema kuwa wanaendelea kujipanga ili kuhakikisha rekodi yao inalindwa ya kuendelea kuongoza kwa ufaulu ambapo mwaka huu lengo ni kufikia asilimia 100.
Aidha uadhimishaji wa mwaka huu umekuwa tofauka na miaka yote kwani wanafunzi wameshindanishwa kwa mitihani na ufaulu kutoka ngazi ya kata hadi wilaya ambapo wamepatikana wanafunzi wanane wataowakilisha kimkoa kwenye mashindano ya elimu.
"Leo tunahitisha mashindano yetu ya wiki ya elimu ambapo leo tumefikia kilele na tumewapata washindi wetu wanane ambao watatuwakilisha kimkoa na tutahakikisha tunafanya vizuri kama mwaka jana", amesema afisa Mageni
No comments:
Post a Comment