Mkurugenzi Msaidizi huduma za uchunguzi wa Wagonjwa Wizara ya Afya Dkt. Charles Massambu amewataka waajiri na Waajiriwa wanaotoa huduma za Maabara kuhakikisha wamesikilizwa na wanafuata taratibu za usajili na kwa yeyote atakayebainika hajafuata taratibu hizo atachukuliwa hatua za kisheria.
Hayo ameyasema leo katika semina fupi ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam ambayo imelenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya huduma za maabara.
Amesema Massambu changamoto zinazoikabili Baraza la Maabara la niwatoa huduma za Maabara na Wataalamu kutoa huduma pasipo kusajiliwa na kukosa leseni ambapo ni kosa la jinai kisheria.
Kwa upande wake Msajili Baraza la afya Theophil Mabiliche amesema baraza linafanya juu chini ili kubaini wanaogushi vyeti frki na mpaka Sasa wamefanikiwa kubaini watu 71 waliogushi vyeti na wanajitahidi kufanya msako Kwa wanaogushi vyeti ili kusaidia wagonjwa kupata huduma ipasavyo.
Aidha amesema Mtaalamu yeyote haruhusiwi kuendesha Maabara ambayo haijasajiliwa kisheria na haruhusiwi Mtaalamu kutoa taarifa ya mgojwa ya majibu ya vipimo vyake bila utaratibu pasipo ruhusa ya mgonjwa au ndugu wa mgonjwa.
No comments:
Post a Comment