• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday 22 May 2018

    Miili ya wafanyakazi watatu wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kuagwa kesho

    Bodi ya wakurugenzi,menejimenti na wafanyakazi wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) wanasikitika kutangaza vifo vya wafanyakazi wenzao watatu Bw.Zackaria Naligia Kingu (kaimu mkurugenzi wa idara ya huduma za kitaasisi),Bw.Said Amri Moshi (kaimu mkurugenzi idara ya utafiti,mipango na mifumo ya mawasiliano) na Bw.Martin Lawrence  Masalu (meneja utafiti) vilivyotokea siku ya jumatatu tarehe 21 mei,2018 kwa ajali ya gari kijijini Msoga,Chalinze,wilaya ya Bagamoyo .

    Hivyo kituo  kinatoa pole kwa wafiwa wote,wanafamilia,ndugu,jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huo.

    Heshima za mwisho kwa marehemu hao zitatolewa katika viwanja vya karimjee jijini Dar es salaam siku ya alhamisi tarehe 24 mei,2018 kuanzia saa nne  asubuh hadi saa saba mchana.

    Baada ya kutoa heshima za mwisho kwa miili hiyo,mwili wa Kingu utazikwa makaburi ya kinondoni saa nane mchana,mwili wa bw.Moshi utasafirishwa kwenda wilayani Karatu na mwili wa bw.Masalu utasafirishwa kwenda mjini Morogoro na maziko yatafanyika siku ya ijumaa tarehe 25 mei,2018.

    BWANA AMETOA,BWANA AMETWAA,JINA LAKE LIHIMIDIWE . AMINA

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI