• Breaking News

    ..

    ..

    Friday 25 May 2018

    Watanzania wenye hati za kusafiria za kielektroniki waaswa kuzitunza vizuri

    Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo, amewataka  wanaopata hati za kusafiria za kielektroniki kuzitunza na kwamba atakayepoteza atalazimika kulipia shilingi laki tano laki  ikiwa ataipoteza kwa mara ya kwanza na shilingi laki saba ikipotea kwa mara ya pili.

    Ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa hati hizo za kusafiria za kielektroniki .


    "Lazima tuzitunze vizuri zisiangukie mikononi mwa watu wabaya, ndugu zangu hatutaki kabisa hati hizi ziangukie mikononi mwa watu wasio raia watanzania"amesema Ndikilo.

    Aidha amesema lengo la kuanzisha hati hizo  ni kukidhi na kuimarisha  usalama wa nchi yetu na utambulisho wa utaifa najua Kenya na Uganda wana pasipoti za namna hii, kwa hiyo tusipozitunza zikaangukia kwenye mikono ya watu wabaya ambao wanaweza kulichafua taifa.

    Kamishna wa Pasipoti na Uraia Gerady Kihinga amesema hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu watakuwa wamekamilisha ufungaji wa mifumo ya uhamiaji mtandao katika katika mikoa yote nchini.

    Pia amesema hadi sasa tayari wamefunga mahojiano ya Dodoma na Dar es Salaam.

    Amesema tangu kuanza kwa kutumika kwa hati hizo za kielektroniki tayari wametoa hati mpya za kusafiria 15101 kote nchini.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI