• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday 24 May 2018

    Mwijage amewataka wafanyakazi wa TIC kuongeza nguvu kazi ili kuziba pengo la wenzao watatu

    Waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji Charles Mwijage amezitaka familia za waliopoteza ndugu,jamaa,marafiki na wafanyakazi wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kuwa wavumilivu kwa tukio la kuwapoteza watu wao wa karibu.

    Akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa kutoa heshima za mwisho  kwa marehemu hao katika viwanja vya karimjee jijini Dar es salaam Mwijage amewaasa wafanyakazi wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kuongeza nguvu kazi ili kuziba pengo la wafanyakazi wenzao watatu waliopoteza maisha.

    "Unapokuwa vitani mwenzako anapoanguka(kufa) unachotakiwa kufanya ni kuchukua silaha aliyokuwa nayo,risasi zilizobaki na kidumu cha maji unamuacha  usilie zaidi,kama familia ikalia na sisi tukilia tutakuwa tunaiangusha nchi pia mm kwangu hawa walikuwa wapiganaji wangu na wapambanaji wangu" amesema Mwijage.

    Kwa upande wa mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffrey Mwambe amesema alipata taarifa ya vifo hivyo vitatu siku ya jumatatu tarehe 21 mei mwaka huu saa 10
    jioni na majeruhi wawili ambao Sasa wapo muhimbili Moi wakati akiwa mkoani mwanza.

    Amesema wanasikitishwa sana na kitendo hiko cha kuondokewa na wafanyakazi wenzao kwani walikuwa ni nguvu kazi katika kituo hiko cha uwekezaji ili kuliletea taifa maendeleo ya kiuchumi.

    Aidha Mwambe amesema bw.zackaria Naligia Kingu (49) ambaye alikuwa kaimu mkurugenzi wa idara ya huduma za kitaasisi atazikwa leo katika makaburi ya kinondoni jijini Dar es salaam,bw.Said Amri Moshi (37) ambaye alikuwa kaimu mkurugenzi idara ya utafiti,mipango na mifumo ya mawasiliano  atasafirishwa kwenda mkoani morogoro kuzikwa kesho tarehe 25 mei,2018 na bw.Martin Lawrence Masalu (39) ambaye alikuwa meneja utafiti atasafirishwa kwenda wilayani Karatu mkoani Arusha na kuzikwa hapo kesho tarehe 25 mei,2018.

    IKUMBUKWE: Wafanyakazi hao wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) walifariki dunia Kwa kupata ajali ya gari wakati wakiwa safarini kuelekea Dodoma siku ya Jumatatu tarehe 21 Mei mwaka huu katika Kijiji cha Msoga,Chalinze,wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI