• Breaking News

    ..

    ..

    Friday 8 June 2018

    Mahakama zimejipanga kuweka mikakati endelevu ya kimaendeleo nchini

    Mahakama za Afrika zinatarajia kukutana kwenye Mkutano mkuu utakaofanyia kwenye Ukumbi wa Kimataifa  Arusha tarehe 11 juni,2018 zikiwa na lengo la kuweka  mikakati endelevu ya kuendeleza maendeleo katika nchi zake.

    Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo Jijini Dar es Salaam, kwenye Mahakama ya Rufaa, Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof Ibrahim Juma, amesema lengo la mkutano huo ni kuzikutanisha Mahakama zote zilizopo barani Afrika kwa ajili ya kuangalia ni kwa namna gani Mahakama zinaweza kuchangia maendeleo katika Mataifa yao.

    Aidha, amesema kuwa katika mkutano huo, wapo miongoni mwa wadau mbali mbali watakaoshiriki , miongoni mwa wadau hao ni pamoja na  Mawaziri wa Sheria, wanasheri, pamoja na wadau wa maendeleo ambao watatoa maada mbali mbali ikiwamo madawati ya kijinsia ambayo ndiyo yatalengwa zaidi.

    Amesema kuwa, mbali na kujadili mipango ya maendeleo pia zipo changamoto zitakazo  jadiliwa na kupatiwa ufumbuzi ili kurahisisha huduma kwa jamii na kutoa haki kwa kila mwananchi.

    Jaji Mkuu, Prof: Juma, amesema Moja changamoto  zinazokabili Mahakama za Tanzania ni pamoja na uchache wa Mahakama ambapo imekuwa changamoto katika kuwafikia wananchi wote kuwapatia huduma kwa usawa.

    Pia amesema kuwa changamoto ya umbali wa vituo, inasababisha wananchi wengi wasio na uwezo kukosa haki kwani ni watu wachache wenye uwezo wa kuzifikia mahakama kwa wakati tofauti na wale wasio na uwezo wanashindwa kusafiri kwa ajili ya kukosa nauli.

    "Tunapoelekea kwenye mkutano wetu yapo mengi tutayazungumza lakini kubwa zaidi kwa upande wetu tumeona ni vyema tukaja na mpango wa  kuzindua huduma mtembeo kwa mabasi(Mobile Service)ambapo   Mabasi hayo  yatakuwa yakitembea sehemu mbali mbali ili  kurahisisha huduma za Kimahakama katika  kumfikia mwananchi kwa harakashia na wale wasio na uwezo wa kuzifikia mahakama wapate fursa hiyo katika kujenga uaminifu wa kiutendaji na wananchi wake""amesema Prof: Ibrahim.

    Kwa upande Wa Makamu wa Rais wa Benki Kuu ya Dunia, MS Sandie Okoro, amesema kuwa, ameridhishwa na utendaji wa Mahakama kuu ya Tanzania, hivyo kama Benki kuu ya Dunia haitasita kuendelea kuwasaidia Tanzania  katika kupiga hatua za kimaendeleo katika kuboresha miundombinu ya Mahakama ili kufanya kazi zake kwa ufanisi.

    "Nimefurahishwa sana na mapokezi yenu, hii ni mara yangu ya kwanza kufika Tanzania nilipota ujumbe tu haraka nikasema lazima nifike tuone maendeleo ya Tanzania katika mfumo mzima wa Mahakama pamoja na changamoto zake, sisi kama wadau wakubwa wa maendeleo tupo  pamoja na tutaendelea kushirikiana katika kuboresha Mahakama zenu"'amesema MS Okoro.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI