• Breaking News

    ..

    ..

    Friday 8 June 2018

    Wawekezaji na wafanyabiashara waaswa kushiriki kongamano la kibiashara Mbeya ili kubaini fursa mbalimbali za kibiashara

    Ofisi ya mkuu wa mkoa wa mbeya kwa kushirikiana na kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC),mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania (TanTrade) na taasisi ya biashara na uwekezaje ya Malawi (MITC) imewataka wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi katika kongamano la wafanyabiashara na uwekezaji mbeya  ikiwa ni lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji hao ili  kubani  fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji zitakazowawezesha kuanzisha na  kuendeleza Miradi katika sekta  za Viwanda ,Usafirishaji,Utalii,Uvuvi,Kilimo,Madini,Elimu,Afya,Benki,Mawasiliano,Tehama,na Biashara kwa Ujumla.


    Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Amosi Makala  amesema  kongamano litafunguliwa na mgeni rasmi makamu wa rais wa jamuhuri ya muunganoMuungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan rather 26 Na na 27 julai,2018 katika ukumbi wa Royal Tughimbe,Mafiati jijini mbeya  na linatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki 500 ikijumuisha wafanyabiashara,wawekezaji,taasisi za umma na sekta binafsi kutoka Tanzania na Malawi.

    Kauli mbiu ya kongamano hilo ni "kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi".

    Wakati Wa kongamano hilo kutakuwepo na mikutano ya wafanyabiashara (B2B), mikutano ya watendaji wa serikali (G2G) na mikutano kati ya serikali na wafanyabiashara (B2G) kutoka nchi hizi mbili.

    "Tayari mkoa wa mbeya umeona umuhimu wa kongamano hili na unakila sababu za kuandaa na kuratibu  kwasababu unaona fursa na mkoa unamiundombinu ambayo ni uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe unatoa fursa kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa nchi za kusini mwa jangwa la sahara kurahisisha usafiri wa abiria na mizigo na barabara za lami zinazounganisha mkoa wa Mbeya na mikoa mingine na nchi za Jirani (Malawi na Zambia)" amesema Makala.

    Pia mesema  serikali  kupitia mkoa wa Mbeya  imeanza kufungua milango ya uwekezaji kwa kuwekeza katika miundo mbinu ya kiuchumi ikiwemo uwepo wa meli mbili za mizigo na moja ya abiria inayotengenezwa katika bandari ya Itungi na kuanza ujenzi wa kituo kimoja cha forodha(one stop boarder post  katika mpaka wa kamusulu.

    Aidha amesema serikali imekwisha tenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa bandari kavu katika eneo la Inyara kwa lengo LA kuwezesha upokeaji na uhifadhi wa bidhaa moja kwa moja kutoka bandari ya Dar es salaam.

    Aidha Amesema kwa wadau wenye nia ya kushiriki kongamano hilo wanahamasishwa kupakua na kujaza fomu ya usajili kupitia tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mbeya www.mbeya.go.tz na kuziwasilisha kwa barua pepe; Ras.mbeya@mbeya.go.tz (simu: +255-2504045 au +255 767  396924), kituo cha uwekezaji (TIC) http://www.tic.go.tz/displayListPublication na kutuma kwa diana.ladislaus@tic.go.tz/ ( simu Na +255 719 653079 au mamlaka ya uendelezaji biashara Tanzania (TANTRADE) kwa tovuti www.tantrade.go.tz kisha kutuma kwa info @tantrade.go.tz  au (simu:+255 767 924, +255 713 274 653) au kituo cha biashara na uwekezaji cha Malawi (MITC) kupitia tovuti, HTTPS://mitc.mw/ na kutuma kupitia infi@mitc.mw au kwa simu namba +265 1 771 315 na ziwasilishwe kabla ya jumatatu tarehe 16 julai,2018.


    Kwa upande wake mkurugenzi wa sekta binafsi   amesema Tazania na Malawi uko kwenye Jumuiya ya  SADEC hivyo SADEC kuna soko lenye Vivutio Vyake itasaidia kupata kwa urahisi kutengeneza Masoko kwa watu mbalimbali.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI