• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday 7 June 2018

    Mataifa 51 barani Afrika kushiriki mkutano wa majaji Arusha ili kuboresha dawati la jinsia

    Mahakama ya Tanzania inatarajia kukutanisha jumla ya Mataifa 51 kutoka barani afrika kwa ajili ya kufanya maboresho ya kutatua kero za madawati ya kijinsia katika bara la Afrika.

    Akizungumza na waandishi wa habari, leo jijini Dar es salaam katika mahakama ya rufaa , jaji kiongozi wa mahakama ya Tanzanania,  Dr Eliezer Feleshi, amesema mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa arusha tarehe 11 hadi 13 , ambapo jumla ya wajumbe 350 watahudhuria mkutano huo huku wajumbe 200 watatoka Tanzania bara na visiwani.

    Aidha jaji Eliezer, amesema lengo la mkutano huo ni kuwakutanisha wadau mbali mbali wakiwemo watunga sera ili kupitia na kufanya maboresho katika madawati ya kijinsia katika kueleta usawa kwa watu wote bila ya ubaguzi jambo ambalo kwa bara la Afrika ni changamoto.

    Amesema kuwa, katika mkutano huo, zipo maada mbalimbali zitakazojadiliwa lakini kila maada itakayojadiliwa itakuwa na mguso wa dawati la kijinsia katika kufikisha ujumbe kwa walengwa na kuwaondolea kero wadau wanaokumbwa na matatizo ya kijinsia na wale wanaonyimwa haki zao.

    Hata hivyo, amesema wao kama mahakama wameona kuna haja ya kuja na mapendekezo maaalumu ambayo yatahitajika kupatiwa ufumbuzi na kuona ni kwa namna gani bara la afrika linaweza kujinasua na changamoto za kesi za kijinsia ili kuleta haki sawa kwa watu wake.

    "Nipende kusema kwamba huu mkutano utaibua mambo mengi sana, tutajadili kwa pamoja changamoto za bara letu la Afrika juu ya madawati ya kijinsia, hivyo baada ya mkutano kumalizika tunaimani tutakuja na njia mbadala za kutatua kesi hizo na maboresho kadhaa ili kusaidia madawati yetu kufanya kazi zake kwa ufanisi wa hali ya juu""amesema jaji Eliezer.

    Kwa upande wa msajili mkuu wa mahakama kuu  ya tanzania, Katarina REVOCATI, amesema  mahakama za Tanzania hakuna changamoto kubwa ya usawa wa jinsia kwani mpaka sasa ni 45% ya maafisa wa mahakama walioajiriwa ni wanawake hivyo kwa takwimu hiyo inaonyesh ni kwa jinsi gani wanasogelea ule usawa wa asilimia hamsini Kwa hamsini.

    Amesema  wapo katika mchakato wa kufanya maboresho kadhaa ambayo yatasiadia kuongeza uwajibikaji wa madawati ya kijinsia katika kufikisha haki sawa kwa watu wote kwa ukaribu na wale amabo hafahamu haki zao watahudumimiwa bila kujali rangi, mazingira, jinsia, dini wala kabila.

    "Huu ni mwanzo wa kuwekaka usawa kwa watu wote, tumekuwa na kesi nyingi sana za jinsia lakini kwa sasa tunapoelekea katika mkutano huo kuna mambo mengi sana tutayaibua na kwa kweli tunazingatia sana usawa na uwiano wa ajira kazini, ajira zinapotangazwa katika mahakama zetu vigezo vikubwa  ni kuangalia sifa, kama wanazo watapata a wale ambao watakosa basi watakuwa wameshindwa kufuzu vigezo vinavyotakiwa"amesema revocati.

    katika hatua nyingine, mahakama hiyo kesho inatarajia kufanya mkutano na mwakilishi kutoka benki ya dunia kwenye mahakama ya rufaa na baada ya mkutano huo mwakilishi huyo atakuwa na ziara ya kutembelea mahakama mpya iliyojengwa kupitia fedha za benki kuu ya dunia iliyoko wilaya ya kigamboni.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI