Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Mhe Samia Suluhu ametoa wito kwa taasisi za kiraia,taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali kushirikiana pamoja mashirika mengine kujitathimini namna ya kuepukana matumizi ya mkaa na kuni badala yake watumie nishati mbadala ili kusaidia Uhifadhi Mazingira.
Wito huo umetolewa Leo Jijini Dar es salaam katika siku ya pili ya wiki ya maadhimisho ya wiki ya mazingira katika kongamano lililokutanisha wadau mbalimbali wa Mazingira na taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali amesema matumizi ya kuni na mkaa husababisha ukataji wa miti hivyo husababisha Uharibifu wa mazingira kwa kiwango kikubwa .
Kongamano hilo limebebwa na kauli mbiu isemayo "MKAA NI GHARAMA TUMIA NISHATI MBADALA".
Kwa upande wake Waziri Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa raisi mazingira na Muungano January Makamba amesema Uchumi endelevu wa Nchi umekuwa kwa kasi kwa Miaka kumi na tano iliyopita lakini Mazingira yameathiriwa kwa kasi hivyo jitihada zinatakiwa zifanyike ili kusaidia kunusuru Uharibifu uliotokea ili kusaidia Mazingira yawe bora zaidi .
Kwa upande wake Balozi wa Swideni Katarina Rangnitt amesema Shunguli za kiuchumi kama kilimo Uvuvi,Ufugaji,zimeathiri Mazingira kwa kiasi kikubwa hivyo inatakiwa mikakati ya ziada itumike kunusuru janga hilo.
No comments:
Post a Comment