• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday 30 May 2018

    Vijana watakiwa kujitambua kuwa wao ni rasirimali watu muhimu kwa maendeleo ya taifa

    Katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu,ofisi ya waziri mkuu-kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Eric Shitindi  amewataka vijana kujitambua kuwa wao ni rasirimali watu muhimu  kwa ajili ya maendeleo endelevu  ya kiuchumi,kijamii kwa taifa.        

    Amesema hayo leo katika ufunguzi wa mkutano wa vijana wa Dar es salaam,pwani na Morogoro Kwa ajili ya kukusanya maoni ya rasimu ya sera mpya ya maendeleo ya vijana uliofanyika jijini Dar es salaam.

    Amesema sera mpya ya maendeleo ya vijana itawezesha kundi kubwa la vijana kushiriki kikamilifu katika utekelezaji malengo endelevu ya dunia ifikapo 2030 katika kiwango cha mtu binafsi,taifa na kimataifa

    "Vijana wanategemewa kufanya mabadiliko ya uchumi wa nchi hivyo lazima wasimame imara katika masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii kwa taif" amesema Shitindi.    

    Pia amesema kulingana na sensa iliyofanyika mwaka 2012 ilionesha asilimia 35 ya watanzania wote ilionesha ni  vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 35 na asilimia 56 ya nguvu kazi ya taifa ni vijana wenye umri huo.        

    kwa upande wa mwakilishi wa shirika la umoja wa mataifa linaloshughulika na idadi ya watu (UNFPA) Tausi Hassan amesema vijana wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama ukosefu wa ajira,kutoshirikishwa katika masuala mbalimbali ya nchi hivyo kupelekea kuwa katika hali duni.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI