
Katika mkutano wa tisa kikao cha sita wabunge mbalimbali waliuliza maswali na kujibiwa na serikali kama ilivyo kawaida, haya ni mambo 9 kwa ufupi yaliyozungumzwa ndani ya Bunge.
#Makusanyo yatokanayo na kodi za majengo kutoka Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji 30 yaliyokuwa yakisimamiwa na TRA yameongezeka kutoka shilingi bilioni 28.28 mwaka 2015/16 hadi bilioni 34.09 kwa mwaka 2016/17 – Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.
#Kodi za majengo kutoka Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji kwa mwaka 2015/16 ilikusanywa na Serikali za Mitaa na mwaka 2016/17 TRA ilianza kukusanya kodi hiyo – Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.
#Ongezeko la makusanyo linadhihirisha kuwa, TRA imefanya vizuri zaidi katika kukusanya mapato hayo ikilinganishwa na Halmashauri hizo 30 katika mwaka 2015/2016 – Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.
#Katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia wanafunzi wenye ulemavu nchini, Serikali imetoa mafunzo kazini kwa walimu 699 wanaofundisha wanafunzi wenye ulemavu wa akili na wenye usonji – Mhe. William Ole Nasha.
#Wizara ya Elimu inakamilisha uandaaji wa mwongozo wa kufundishia wanafunzi wenye ulemavu wa akili na wenye usonji ambao utasambazwa katika vitengo 349 vinavyopokea wanafunzi hao – William Mhe. Ole Nasha.
#Mwongozo huo unalengo la kupanua uelewa wa walimu juu ya mbinu za kufundishia, matumizi ya vifaa pamoja na saikolojia ya kufundishia wanafunzi hao – William Mhe. Ole Nasha.
#Maafisa Maendeleo ya Jamii walikuwa wakitumika kama spare tire katika Halmashauri. Lakini kuanzia sasa tumewapa mwongozo wa kuwafikishia wakurugenzi wao ili waweze kuwatumia – Mhe. Selemani Jafo.
#Kuanzia sasa mtaona mwenendo tofauti wa utendaji wa Maafisa Maendeleo ya Jamii chini ya Wizara ya Afya pamoja na TAMISEMI ambao wanawasimamia kwa ukaribu – Mhe. Selemani Jafo.
# Maafisa Maendeleo ya Jamii ndio injini ya mabadiliko katika Halmashauri – Mhe. Selemani Jafo.
CHANZO BONGO 5.COM
No comments:
Post a Comment