Kocha huyo Mhispania juzi aliiongoza Azam kwa mara ya kwanza katika mechi ya kimashindano ambapo ilishinda kwa mikwaju ya penalti 4-1 baada ya mechi kumalizika kwa sare ya mabao 2-2. Akizungumza na gazeti hili, kocha huyo alisema anakichokifanya kwa sasa ni kuhakikisha wachezaji wake wanamuelewa.
“Kama wachezaji wangu wakinielewa kile ninachowafundisha basi sina wasiwasi na mataji mengine kwenye soka ya Tanzania, ninao uwezo wa kuyabeba yote,” alisema.
Azam imetwaa Ngao ya jamii kwa mara ya kwanza baada ya kuikosa karibu mara mbili na sasa ina kazi ngumu ya kuwania taji la Ligi Kuu bara na lile la Kombe la FA. Kauli hiyo iliungwa mkono na nahodha wa timu hiyo John Bocco ambaye alisema ushindi huo unatoa ishara hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi Bocco alisema anashukuru kwa kupata ushindi huo na sasa wanajipanga kupambana kwenye ligi ili kushinda katika michezo ijayo.
“Tunashukuru tumepata ushindi wetu kwa kwanza msimu huu, inaonesha kuwa mambo mazuri yanakuja mbele, msimu huu ni zamu yetu kuchukua taji la ubingwa,”alisema.
Kikosi hicho kinaendelea na kambi yake Chamazi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kwanza utakaochezwa kesho dhidi ya Afican Lyon.
No comments:
Post a Comment