• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 16 September 2016

    Aliyetorosha mabinti wanafunzi jela




    MAHAKAMA ya Wilaya ya Singida imemhukumu mkazi wa kijiji cha Mkimbii, Ilongero wilayani Singida, Tatu Ntandu (49) kwenda jela miaka ninne kwa makosa ya kutorosha na kukatisha masomo wanafunzi wawili wa darasa la saba.
    Ntandu anadaiwa kuwatorosha Hawa Mussa (13) na Rauza Athumani (13), wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtipa katika Manispaa ya Singida.
    Aidha, mahakama hiyo imemwamuru kulipa faini ya Sh 40,000 mara atakapomaliza kutumikia kifungo gerezani.
    Mwendesha Mashitaka, Patricia Mkina, alidai mbele ya Hakimu, Flora Ndale, kuwa Aprili 5 mwaka jana, saa 5.00 asubuhi katika kijiji cha Mtipa, Manispaa ya Singida, mshitakiwa Ntandu, bila makubaliano na wazazi wa wanafunzi hao, aliwatorosha na kuwapeleka kusikojulikana wanafunzi hao.
    Ilidaiwa mahakama hapo kuwa siku ya tukio, mshitakiwa alifika nyumbani kwa mzazi wa Hawa, Mussa Swalehe, baada ya kusalimiana na kufanya mazungumzo ya kawaida, Swalehe alitoa mifugo yake kwa ajili ya kupeleka machungani.
    Mkina alidai kuwa, Mussa aliporejea nyumbani jioni, hakumkuta mtoto wake na rafiki yake Rauza, ambaye aliwaacha wakati alipoenda kuchunga na hapo ndipo alipowajulisha majirani na msako mkali wa kumtafuta Ntandu na wanafunzi hao ulipoanza.
    Akitoa hukumu, Hakimu Ndale alisema upande wa mashitaka umethibitisha bila kuacha shaka yoyote kwamba mshitakiwa Ntandu ana hatia kama alivyoshitakiwa; hivyo anapewa kifungo cha miaka minne jela na kulipa fidia ya Sh 20,000 kwa kila mwanafunzi.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI